Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya 4 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilosa mkoani Morogoro, Mustafa Haidi Mkulo mapema Leo mazishi yake yamefanyika nyumbani wilayani Kilosa.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stagomena Tax, Waziri nchi ofisi ya Rais Mhe George Mkuchika, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima, Washauri wa Rais Mhe Bulembo na Mhe Lukuvi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa umma Mhe Ridhiwani Kikwete, Mkuu wa JKT, Jaji mfawidhi Mkoa Morogoro.
Wakurugenzi wa taasisi na Mashirika ya Umma, Viongozi wa CCM wakiongozwa na Mkti wa CCM Mkoa wa Lindi na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, na Mwenyeji wake Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mh Shaka Hamdu Shaka, wabunge wote wa majimbo mawili ya Kilosa Mh. Palamagamba Kabudi wa Kilosa na Mh. Denis Londo wa Mikumi na viongozi mbali mbali waandamizi wa Chama na Serikali, viongozi wa dini pomoja na mamia ya wananchi kutoka katika maeneo mbali mbali nchini.
Marehemu Mustafa Mkulo amezikwa katika makaburi ya Kimamba Wilayani Kilosa