Na Prisca Libaga Arusha
Ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, Mei 4, 2024 imeshiriki Matembezi ya Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani.
Maadhimisho hayo yameratibiwa na Asasi ya Kiraia ya Self Awareness for Everyone (SAFE) inayoendesha shughuli zake katika Jiji la Arusha.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hao alikuwa Mganga wa Mkoa wa Arusha Dk. Charles Mkombachepa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda.
Matembezi ya Maadhimisho hayo yalianzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhitimishwa katika Viwanja vya Gymkhana Jijini Arusha.
Dawa za Kulevya Husababisha Changamoto ya Afya ya Akili.