Na. Mwandishi wetu, Katavi
Wafanyabiashara katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi wameishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
Wafanyabiashara hao wametoa shukurani hizo katika semina ya iliyofanyika katika kata ya Maji Moto iliyolenga kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara, kupitia kampeni ya mlango kwa mlango inayolenga kuwaelimisha wafanyabiashara juu ulipaji wa kodi.
“Elimu tuliyopata itatusaidia sana kwani imetuongezea ujasiri” alisema Johari Ali mmoja wa wafanyabiashara.
Ameeleza kuwa katika semina hiyo amejifunza umuhimu wa kufanya biashara kwa kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi.
Katika hatua nyingine ameiomba TRA mkoa wa Katavi kuendelea kutatua changamoto za wafanyabiashara katika kata ya Maji Moto kwa lengo la kujenga uhusiano mwema katika kulipa kodi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kavuu Geophrey Pinda amewaomba kuendelea kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa kuwa kodi huisadia serikali kujenga miundombinu mbalimbali.
Pinda ametoa wito kwa TRA kujenga mahusiano mazuri kwa wafanyabiashara wa Majimoto kwani uchumi wa wananchi unategemea wafanyabiashara.
“Mimi kama mbunge wa Jimbo la Kavuu nitawapa ushirikiano sana TRA lakini ushirikiano huo huo uende sambamba na mahusiano mazuri ya wafanyabiashara” Pinda.
“Niwajibu wangu kuhakikisha maisha ya wafanyabiashara haya bugudhiwi kwa sababu ya kodi wakati naingia hapa mkurugenzi hata kodi za Halmashauri zilikuwashida” Pinda.