Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha,Blandina Nkini akizungumza katika kongamano hilo mkoani Arusha.
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Wanawake kutoka jamii za pembezoni za kifugaji wameshauriwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza na kushiriki matukio katika jamii ikiwa ni pamoja na kuwa mstarinwa mbele katika kugombea ngazi za uongozi.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Afisa maendeleo ya jamii Blandina Nkini wakati akifungua kongamano la wanawake wa jamii za kifugaji linalofanyika hapa mkoani ambapo amewataka kujitokeza kushiriki ngazi mbalimbali za maamuzi ili kuweza kutokomeza ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike kufanyiwa ukeketaji.
“Nawaomba sana wanawake kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao bila kujali mila na desturi zinazowazuia kwani nao wana wajibu mkubwa wa kutumia nafasi zao kikamilifu katika kiwanja nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao.”amesema .
Aidha amesema kuwa,uwepo wa kongamano hilo kwa wanawake hao ni jambo zuri sana kwani linawakumbusha wajibu wao wa kugombea nafasi mbalimbali na kuwa na udhubutu bila kuogopa mila na desturi zilizopo katika jamii yao.
Kwa upande Afisa jinsia kutoka shirika la Pingo’s Nailejileji Tipap amesema katika kongamano hilo wamekusanya wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya pembezoni lengo likiwa ni kuwatengenezea uelewa na kutambua haki zao za msingi.
Amesema kuwa,kupitia kongamano hilo wanawake hao wanajengewa uelewa wa kutosha wa kuweza kutambua haki zao za msingi .
Amefafanua kuwa , katika jamii wanazofanya nazo kazi bado kuna Mila na desturi ambazo zinaendelea kuwakandamiza wanawake na kuwanyima usawa katika kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa,katika jamii nyingi za asili bado kuna mila zinazoendelea kuwakandamiza wanawake ikiwemo maswala ya ukeketaji jambo ambalo bado ni changamoto kubwa kwa jamii husika.
“Wanawake wengi wamekuwa wakijiona kuwa hawana nafasi katika uongozi kutokana na mila na desturi zinazowabana jambo ambalo bado limekuwa ni changamoto kubwa, hivyo kupitia kongamano hilo wanawake wataweza kutambua nafasi zao na kuondoa hofu katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani ni wajibu wao kufanya hivyo.”amesema .
Kwa upande wake Nalemuta Moisan kutoka shirika la PWC , amesema lengo la kuwakutanisha ni kuibua maswala mbalimbali na changamoto wanawake hao wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kufanya maamuzi .