Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko (kushoto) akimpatia tuzo ya EWURA, Ofisa wa EWURA anayehusika na ushirikishwaji wa wazawa katika Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia nchini, Bw. Joseph Mboma (wa pili kulia).
Mchumi kutoka EWURA,Bw. Joseph Mboma,akiwa ameshika ngao na cheti kilichotolewa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) baada ya kuwa mshindi wa pili katika usimamizi wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwenye mkondo wa kati na wa chini wa sekta ya mafuta na gesi asilia nchini.
…….
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepokea tuzo ya mshindi wa pili katika Usimamizi Bora wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika Miradi ya Kimkakati Nchini. TANROADS imechukua nafasi ya kwanza huku TAA ikiwa ya tatu.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko wakati wa kongamano lililofanyika tar 28.04.2024; Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini ambao ni EWURA, PURA, TANROADS, TAKWIMU, Tume ya Madini, TIRA, Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere(JNHPP), Wizara ya Maliasili (kupitia mradi wa REGROW), PPRA, IRDP, EACOP, ERB, CRB; asasi za kiraia na taasisi za fedha.