Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF Bw.Neville Meena akizungumza na Waandishi wa habari Leo Aprili 28,2024 kuhusu Mkutano wa kitaaluma wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) utakafanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Mwandishi Mkongwe na Mwanachama wa TEF Bw. Said Salim Said,akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari kuelekea Mkutano wa kitaaluma wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) utakafanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuongoza mkutano wa kitaaluma wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) utakafanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma hukh mada mbalimbali zikitarajiwa kujadiliwa ikiwemo suala la ukuaji wa Teknolojia.
Hayo yameelezwa leo Aprili 28,2024 Jijini Dodoma na Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF Neville Meena wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Mkutano huo ambapo amesema kuwa kwasasa dunia inakumbana na mabadiriko makubwa ya matumizi ya Akili mnemba.
“Kama mnavyofahamu Teknolojia zimekuwepo sasa na ukizikimbia utajikuta uko nje ya dunia na vyumba vyetu vya habari haviwezi kufanya kazi pasipo kuzingatia kwamba kuna mabadiriko makubwa ya Teknolojia,”amesema.
Aidha ameongeza kuwa mada nyingine watakayoenda kujadili ni kuhusiana na matumizi sahihi ya gesi kwaajili ya kulinda misitu ili kuendelea kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini na kusababisha adhari kubwa katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
“Kuma mahusiano makubwa kati ya mabadiriko ya tabia ya nchi na uharibifu wa mazingira ambayo yanaharibu mali za watu, fedha na vitu vingine kwahiyo tumefikilia hiinitakuwa mada yetu kuu katika mkutano wetu ili tunarudi katika vyumba vyetu vya habari tuwe na kitu cha kuandika kwaajili ya kuelimisha umma, kuhamasisha sisi wenyewe lakini kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupigia kelele sana matumizi ya gesi na uhifadhi wa mazingira,”amesema.
Kwa upande wake Mwandishi Mkongwe na Mwanachama wa TEF Bw. Said Salim Said amewataka waandishi wa habari kuelekea uchaguzi wa mwaka huu na ule wa mwakani kuwa daraja la amani na kuepuka kuandika habari zenye uchochezi zinazoweza kuvuruga amani.
“Kwasababu hizi kauli zinazotoka kwenye uchaguzi baadhi yake zinaleta maafa katika nchi yetu, kwahiyo tujitahidi wakati wote tusione ushabiki lakini kubwa zaidi tunachotaka ni tuichangie kuisaidia nchi hii kuvuka salama katika uchaguzi,” amesema.
Adha ametumia wasaha huo kuwaomba waandishi kabadirika katika uandishi wao kwani wengi wao kwasasa aina ya uandishi imekuwa ikifanana na kushindwa kutumia ufundi katika kuwasilisha habari zao kwa jamii.