Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na Usalama, Mmiliki wa eneo hilo na Uongozi wa Serikali ya Mtaa wameteketeza Kijiwe Maarufu cha Matumizi ya Dawa za Kulevya kinachojulikana kama _”JUMBA LA DHAHABU”_ kilichopo Mtaa wa Tindiga, Kata ya Unga Limited jijini Arusha.
Jumba hilo lilikuwa likitumika kwa matumizi na makazi ya waraibu kwa muda mrefu wa dawa za kulevya. Waraibu hao walikuwa wanakutana na kuvuta pamoja na kujidunga dawa za kulevya. Hivyo, Mmiliki na DCEA Kanda ya Kaskazini kuamua kuteketeza jumba hilo itasaidia kupunguza tatizo la dawa za kulevya katika eneo hilo.