Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Uchambuzi na Mapendekezo ya hoja za NHIF na Pensheni nchini Tanzania.
Na Alex Sonna-DODOMA
CHAMA Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU)kimependekeza Kikokotoo kifanyiwe mabadilko kwa kuongeza umri baada ya kustaafu toka miaka 12.5 hadi 15.5 na wanachama wapewe angalau 50% kama mafao ya mkupuo.
Mapendekezo hayo yametolewa Leo Aprili 24,2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa THTU Taifa,Dk Paul Loisulie wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
Dkt.Loisulie amesema kuhusu hoja ya Kikokotoo kinachotumika hakiakisi hali halisi ya wanachama – kanuni 8(1)(a)(b)(c) (a) kigezo cha umri (b) kigezo cha malipo ya mkupuo mapendekezo yao ni Kikokotoo kifanyiwe mabadilko kwa kuongeza umri baada ya kustaafu toka miaka 12.5 hadi 15.5.
Pia wanachama wapewe angalau 50% kama mafao ya mkupuo itumike 1/540 badala ya 1/580.
Kuhusu Waziri husika kuwa na mamlaka ya kuamua kiwango cha michango ya mwanachama katika mfuko wanapendekeza Kifungu kidogo cha 18(2)(b) kiondolewe.
Amesema Waziri hapaswi kuwa na mamlaka ya kupanga michango ya wanachama.
Kuhusu Baada ya kifo cha mwanachama, wategemezi wake hunufaika kwa muda wa miaka mitatu pekee kutoka tarehe ya kifo cha mwanachama THTU inapendekeza Mgane/mjane/mtoto alipwe kwa kutumia kanuni ya mafao kama ilivyo kwa mwanachama wa mfuko angalau kwa miaka 15.
Kuhusu Mwanachama kupunjwa mafao kwa kosa la mwajiri wanashauri Kiongezwe kifungu kidogo
maalum kitakacholinda haki za mwanachama moja kwa moja iwapo mwajiri atachelewesha au kutopeleka mchangowa mwanachama katika mfuko
Ameyataja mapendekezo mengine ni Neno until “re-marriage” linapaswa liondolewe kwenye kipengele (a) ili kulinda haki ya kikatiba ya kuoa na kuolewa pasipo na vikwazo.mjane/mgane aruhusiwe kupata
mafao bila ya vikwazo vya umri na kuwa na mtoto.
Pia,Mwanachama alipwe mafao yake yote na mfuko umdai mwajiri michango iliyokosekana pamoja na penalti.