Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akitoa hotuba katika Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Na Ali Issa. Maelezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi amesema Muongozo malum wa uekezaji Zanzibar SDG utaifungua Zanzibar kiuwekezaji na kuleta mabadiliko ya Uchumi.
Akizungumza kwa niaba ya Rais huyo huko katika ukumbi Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othaman Massoud Othman wakati wa uzinduzi wa mpango wa huo, ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema mpango wa SDG utatoa vipaombele kwa wawekezaji na kuweza kutambua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha amesema mpango huo, utakuwa endelevu na umeweka bayana vichecheo vya uwekezaji ambavyo vitawafanya waekezaji kuchagua fursa wanazozihitaji na kuweza kuwekeza.
Hata hivyo amewapongeza washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la maendeleo la umoja mataifa UNDP kwa ushirikiano wao mkubwa jambo ambalo limepelekea nchi kupiga hatua kimaendeleo na kutimiza malengo ya yaliowekwa na ZADEP ya 2030 na yale malengo ya 2050.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais kazi,Uchumi na uekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff amesema kuzinduliwa mpango huo, inaonyesha kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa kimaendeleo ambapo Serikali imeweka matumaini ya kupokea wawakezaji wengi zaidi.
Sambamba na hayo amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuwapa miongozo ambayo itapelekea Zanzibar kuwa imara katika sekta ya Uchumi na uekezaji.
Nae Mwakilishi Mkazi UNDP Nchini Tanzania Bw. Shigeki Komatsubara amesema Zanzibar itanufaika kutokana na mpango huo sambamba na kuonyesha njia kwa wawekezaji kufika Zanzibar na kunyanyua Uchumi wa nchi.
Mbali na hayo amesema UNDP itaendelea kuisaidia Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa kuiunga mkono katika harakati mbalimbali za kimaendeleo kama nchi nyengine washirika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania Shigeki Komatsubara akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akitoa hotuba katika Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akitoa hotuba katika Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji na Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akikata utepe katika Vitabu kuashiria Uzinduzi wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa(SDG INVESTOR’S)katika hafla ya Maadhimisho ya Sherehe ya Uwekezaji iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.