NJOMBE
Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika amekabidhi gari wagonjwa kituo cha afya Makowo kilicho halmashauri ya mji wa Njombe kilichogharimu zaidi ya mil 560 katika ujenzi hadi kukamilika kwake
Akizungumza na wakazi wa kata ya Makowo katika hafra ya makabidhiano ya gari hilo la wagonjwa mbunge Mwanyika amesema serikali imetoa gari hilo baada ya kukamilisha kituo hicho ili kumaliza changamoto ya usafiri kwa wagonjwa ambao wanatumia fedha nyingi kukodi magari binafsi kwenda hospitali.
Aidha mbunge huyo wa Njombe mjini amesema kwakuwa serikali ya Mama Samia imeona changamoto hiyo na kisha kuamua kutoa gari hivyo kila mwananchi wa kata hiyo anajukumu la kuifatilia na kuhoji endapo ataona likitumika kinyume na kusudio la serikali la kubeba wagonjwa
“Niwatake watumishi na wananchi kulinda gari hili ili lilete manufaa kwa wananchi wa kata ya Makowo na niwatake mtoe taarifa kwa mtendaji,diwani,halmashauri na Mbunge pindi mkiona linatumika vibaya na sisi tutachukua hatua,alisema Mwanyika “
Awali mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dr Jabir Juma amesema serikali imetoa gari kwa kituo hicho ili kurahisisha usafiri kwagonjwa kwasababu wengi wao wamekuwa wakikodi magari na pikipiki kwa gharama kubwa na kuwafanya baadhi kushindwa kumudu.
Dr Juma amesema ujio wa gari hilo na kukamilika kwa kituo hicho kipya cha afya kutasaidia kupunguza vifo visivyo vya lazima vya akina mama,watoto na wagonjwa wengine hivyo mbali na kutatua changamoto hiyo serikali inaendelea na maboresho ya huduma nyingine kama wauguzi,vifaa na dawa.
Nao baadhi ya wakazi wa kata ya Makowo akiwemo Finanzia haule wameishukuru serikali kwa kuwapa gari la wagonjwa kwasababu kwa muda mrefu wameteseka kufata matibabu hospitali za Kibena,Lugarawa,Ikonda na Uwemba huku wakilazimika kubeba wagonjwa katika machela za miti na wengine kubebwa kwenye bodaboda.
Wananchi hawa wasema serikali imewaondoa kwenye tatizo ambalo limewatesa tangu uhuru hivyo wanacho kiahidi ni kuendelea kuwa waaminifu kwa serikali iliyopo madarakani.
Nae askofu wa jimbo katoriki Njombe Ausebius Kyando ameguswa na maboresho makubwa yanayoendelea kufanya na serikali katika sekta mbalimbali hususani afya na kisha kubariki kituo cha afya Makowo na gari la wagonjwa ili viwezei kutumika ipasavyo na kuleta tija kubwa kwa wananchi.
Mara baada ya ukaguzi Askofu Kyando akawataka wauguzi na watumishi wote kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kudai kwamba ni shauku yake kuona vifo vinapungua ama kutoweka katika kata hiyo ya makowo.