Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akimkabidhi mwanzilishi wa Maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo iliyopo Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa mwazilishi wake,Jennifer Dickson (katikati) hundi yenye thamani ya dola 10,000, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam .Msaada huo umetolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (kushoto) ni Mjumbe wa kamati ya maktaba hiyo Gloria Munthali.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa taasisi ya Mwangaza ( OMCW), Marshalo Chikoleka, (kushoto) hundi yenye thamani ya dola 10,000, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam .Msaada huo umetolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (katikati) ni Mtaalamu wa Afya na lishe kwa watoto wenye utapia mlo kutoka shirika hilo Loyce Njilla.
Wanufaika wa msaada wa fedha za msaada wa NVeP wakipatiwa maelezo ya sera za Barrick kusaidia miradi ya kijamii katika hafla hiyo.
Mtaalamu wa Afya na lishe kwa watoto wenye utapiamlo kutoka shirika Mwangaza Loyce Njilla, akionyesha hundi ambayo taasisi yao imepatiwa kwa ajili ya kusaidia kuboresha lishe ya watoto wakati wa hafla hiyo.
Mwanzilishi wa Maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo iliyopo Mwanga mkoani Kilimanjaro, Jennifer Dickson akifurahia hundi ya msaada wa kuboresha maktaba hiyo kutoka NVep na Barrick.
Viongozi wa Barrick nchini katika picha ya pamoja na wanufaika wa msaada wa fedha za NVep wakati wa hafla hiyo.
**
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za Kimarekani 20,000 kwa taasisi zisizo za Serikali za Mwangaza OMCW na Maktaba Jamii ya Martha Onesmo kwa ajili ya kukabilliana na changamoto za elimu na afya katika jamii zenye mazingira magumu.
Martha Onesmo ni maktaba ya kijamii iliyoanzishwa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwezesha jamii kupata huduma za kupata elimu kupitia maktaba hiyo na taasisi ya Mwangaza OMCW iliyopo jijini Dar es Salaam inajishughulisha na kuwezesha wanawake kiuchumi,elimu na afya ya motto (Mother&Child in Health).
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido, amesema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.
“Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 15 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP ,lakini huu ni mwanzo,leo tuko hapa kuleta mabadiliko katika taasisi mbili kwa kuzipatia msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kila moja kwa ajili ya kuboresha elimu na afya na lishe kwa watoto katika jamii ’’, amesema Ngido.
Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mwanzilishi wa maktaba ya Jamii ya Martha Onesmo, Jennifer Dickson, ameshukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kuboresha huduma za maktaba hiyo kuwa za kisasa zaidi kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani kote.
Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Mwangaza(OMCW),Marshalo Chikoleka, ambaye alipokea hundi kwa niaba ya taasisi hiyo , ameshukuru kupatiwa msaada huo na amesema kuwa utasaidia kuboresha huduma kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji ambayo taasisi hiyo inahudumia,fedha hizi zinatasaidia kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto kupitia lishe bora ,elimu na kuwezesha wanawake kiuchumi.