Waziri wa ujenzi , mawasiliano na uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohammed Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga huko uwanja wa ndege vya Abeid Amani Karume Zanzibar.
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya viwanja vya ndege Seif Abdalla Juma akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano ulioelezea maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga huko uwanja wa ndege vya Abeid Amani Karume Zanzibar.
Waziri wa ujenzi , mawasiliano na uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohammed akifanya ziara maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege vya Abeid Amani Karume Zanzibar ikiwemo ujenzi wa terminal 2 ili kuangalia maendeleo ya ujenzi huo .
PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR
Na Takdir Ali. Maelezo.
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema Serikali imepata mafanikio ya kiuchumi kupitia mpango wa mageuzi wa sekta ya Anga.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiuana na maendeleo ya sekta ya anga katika Ofisi za Mamlaka hiyo amesema hatua hiyo imesaidia kuongezeka meli za kimataifa na kufikia abiria milioni 1.9 mwaka 2023.
Amesema kutokana na utoaji wa huduma bora katika viwanja vya ndege, ukusanyaji wa mapato umeongezeka na kufikia sh. 29.3 sawa na asilimia 152 ukilinganishwa na mwaka 2019.
Aidha amesema kupitia Kampuni ya Emirate leisure Retail, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zabzibar ulipata tuzo ya kiwanja bora kilichofanya mabadiliko makubwa katika huduma ya vyakula katika jengo la tatu la abiria ambapo ilitolewa September 2023.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Malamaka ya viwanja vya ndege Zanzibar Seif Abdallah Juma amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya pamoja na kuimarisha mfumo wa kuhudumia abiria.
Hata hivyo amewaomba Waandishi wa habari kushirikiana na mamlaka hiyo ili wananchi waweze kujuwa maendeleo yaliopatikana kutokana na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.