Na Paul Mabeja,LINDI
Mbunge wa kuteuliwa Riziki Lulida amelipongeza Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) kwa kufutulisha watu wenye ulemvu pamoja na makundi mengine yenye uhitaji katika mkoa wa Lindi.
Lulida, ametoa pongezi hizo leo Aprli 6 katika viwanja vya Ilulu mkoani hapa, mara baada ya kukamilika kwa tukio hilo la kufutuliasha waumini wa dini ya kiislamu wenye ulemavu pamoja na makundi mengine yenye uhitaji.
Amesema anaipongeza STAMICO, kwa kuwezesha tukio hilo kufanyika katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni sehemu ya moja ya ngozo ya Uislam.
“Tukio hili la kufutulisha watu wenye mahitaji maalum ni sehemu ya kuonyesha upendo baina yetu lakini pia ni sehemu ya swawabu mbele za Mungu hivyo naishukuru sana STAMICO kwa kusaidi kufutulisha kundi hili la wenye mahitaji maalum”amesema
Aidha, ametoa wito kwa watu wenye uwezo na mashirika mengine kujitolea kusaidia watu wenye mahitaji maalum ambao hawana uwezo wa kupata futali katika kipindi hicho cha funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shekhe wa mkoa wa Lindi Mohamed Mushangani, amemshukuru Mbunge Lulida kwa kuwezesha shirika la STAMICO kusaidia kugharamia futali kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum wa mkoa huo.
“Pamoja na majukumu yake mengine ya kibunge lakini mbunge Riziki Lulida amekuwa msatali wa mbele kusaidia watu wengine katika jamii yake wakiwemo wenye mahitaji maalum”amesema
Mkurugenzi wa Shirika la Foundation For Disabilities Hope (FDH) Maiko Salali amesa tukio hilo lililoratibiwa na Mbunge Lulida chini ya ufadhili wa STAMICO, linaonyesha ni kwa namna gani ambavyo amekuwa akishirikiana na jamii katika hali zote bila kujali majukumu yake makubwa aliyonayo.
“Tunamshukuru sana mama Lulida kwa tukio hili ambalo amelifanya leo kwa watu wenye mahitaji maalum hii inaonyesha ni kwa namna gani alivyo mtu wa watu bila kujali majukumu yake makubwa ya ubunge aliyonayo”amesema Salali