Wana Chalinze wa Tarafa za Kwaruhombo na Msata wamejumuika na Mbunge wao ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete katika futari ya pamoja kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani.
Futari hii iliyokutanisha Masheikh na waumini mbalimbali ilitumika pia kumuombea Rais wa JMT Dr. Samia Suluhu Hassan na kufanya kumbukizi ya miaka 25 toka kufariki kwa Mama Mzazi wa Baba yetu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete , Bibi Goya Bint Jumbe. Tunawashukuru sana kwa kuja.