WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe,akisisitiza jambo kwa washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.David Silinde ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Pamba Tanzania Christopher Mwita Ghachuma,akitoa taarifa ya Maendeleo ya Tasnia ya Pamba wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda,akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa inayolima wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM)Mhe.Stanslaus Nyongo,akizungumza kwa niaba ya wabunge wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wakuu wa Mikoa wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika leo Machi 23,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Kilimo Hussen Bashe amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Sekta ya Pamba inaendelea kukua kutoka kuzalisha Tani 174 , 486 Hadi kufikia 282510 kwa Mwaka 2022/2023.
Waziri Bashe ameyasema hayo leo Machi 23,2024 wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika jijini Dodoma
Amesema kuwa kuongezeka kwa uzalishaji huo kunatokana na dhamira ya serikali ya Awamu ya Sita kutoa kipaumbele katika sekta ya kilimo.
“Uzalishaji wa zao la pamba umeendelea kuongezeka nchini hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dk.Samia kwasababu ameonyesha nia ya kukifanya kilimo kuwa ndio uti wa mgongo wa Taifa kwa kuongeza bajeti ya kilimo ili kuhakikisha pembejeo zote za zinapatikana,”amesema
Aidha amesema kuwa Msimu wa kilimo wa mwaka 2012/2022 uzalishaji wa pamba ulikuwa tani 174,486 lakini kutokana na uwekezaji uliofanyika kuanzia ongezeko la bajeti vimechangia uzalishaji kuongezeka hadi kufikia tani 282,510 kwa msimu wa mwaka 2022/2023,.
Hata hivyo Mhe.Bashe amesema kuwa katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ya Kilimo itatoa shilingi milioni 10 kwa Kila Mkuu wa mkoa na shilingi milioni 5 kwa kila mkuu wa Wilaya lengo likiwa ni kuwafanya waweze kufuatatilia shughuli za Kilimo hapa nchini.
Aidha amesema kuwa katika bajeti hiyo watagawa magari na kujenga nyumba kwa maafisa ugani ambapo kwa bajeti hiyo pia wataoa magari 50 kwa maafisa Kilimo mkoa na maafisa Kilimo wa wilaya .
“Wizara inakwenda kujaza mafuta pikipiki za maafisa ugani lengo ni kuondoa malalamiko ya kutokwenda kwa wakulima mashambani kwa kigezo cha kukosa mafuta na kwa hatua hiyo sasa tupo kwenye usajili wa wakulima tu nataka kujua mpaka sasa tuna wakulima wangapi na tunawasaidiaje uzuri baadhi ya wakulima wanaendelea kufanya usajili, “amesema Waziri Bashe.
Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini (TCB) Marco Mtunga amesema Uzalishaji wa pamba baada ya msimu wa bei 2019 /20 walizalisha 348.77 baada yakupata hapo uzalishaji ulishuka baada ya mwenendo wa bei na wakulima walivyoweza kipata shida wakati ule.
Baada ya kushirikiana na maelekezo ya Waziri wameweza kufanya mabadiliko makubwa na uzalishaji umeweza kufikia tani 282000 msimu huu tunaoishia
“Vita kubwa tunayoendelea nayo ni kwamba mazao mengi likiwemo zao la pamba tija iko chini ndio tunapambana kuweza kurekebisha hiyo kasoro ili uzalishaji wa pamba uweze kuongezeka na Pato la mkulima kuongezeka, “amesema .
Amesema kwa sasa iko hivi mkulima anayezalisha kilo 200 pato lake ni dogo ukilinganisha na mkulima anayezalisha kilo 1000.
“Chakwanza tunachokwenda kukifanya mkulima ana kwenda kupanda kwa vipimo ili kupata idadi ya miche sahihi inayotakiwa kwenye eneo na kuboresha huduma za ugani ili elimu kwa matumizi ya viwatilifu na upandaji na shughuli zote za Kilimo ziweze kusimamiwa kwa karibu zaidi, ” Amesema.
Na kuongeza “Tumeweza kusajili wakulima wawezeshaji zaidi ya 5000 ambao wapo karibu kila kijiji hao watatengeneza mtandao wa utoaji wa huduma za ugani kwamana badala ya afisa Kilimo mmoja kwenye kata watakuwa na watendaji wengine Saba hadi 10 ambao ni wakulima wanaozalisha vizuri nayo itasaidia Serikali kuajiri maafisa Kilimo wengi.
Akiongelea suala la maafisa ugani kutofika kwa wakulima kwa kigezo cha pikipiki kukosa mafuta amesema ni kweli pikipiki zimesambazwa kila sehemu na wakurugenzi watendaji wametakiwa kusambaza mafuta ili maafisa ugani waweze kufanya kazi lakini Serikali imekuja na jambo jema kwa wakulima ambapo kwa Mwaka huu wafedha Serikali inakwenda kutenga fedha ya mafuta ya pikipiki kwa maafisa Kilimo kuweza kufanya kazi bila shida yoyote.
Naye Mwenyekiti wa Bodi Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania Christopher Mwita Ghachuma, Amesema kwenye sekta ya Pamba kumekuwepo na matatizo mengi ambayo mengine wanayamudu kuyatatua na mengine yapo nje ya uwezo wao
” Tunaiomba serikali yetu sikivu zile changamoto tunazoshindwa kuzitatua hasa sisi wakulima wa Pamba itusaidie ili tuone tija ya ukulima wetu, “amesema