Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati akifunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Jijini Dodoma.
Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa (katikati) akijibu hoja zilizowasilishwa na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Muundo na mgawanyiko wa majukumu wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Afisa Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Edwin Bilikundi akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu utaratibu wa kuendesha mashauri ya nidhamu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi yake mara baada kufunga kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada ya kufunga kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria kutoka katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kutoa ushauri mahususi kwa Maafisa Masuuli wao ili kuepuka kuipa hasara Serikali.
“Ninajua kusimamia rasilimaliwatu sio jambo jepesi kwani linahitaji hekima na busara. Wapo baadhi ya Maafisa Masuuli ambao hawasikilizi na hawapendi kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maofisa wao na hivyo kutoa uamuzi kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo kuipa hasara Serikali” amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, iwapo sheria na kanuni za usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma hautazingatiwa, utaondoa adhima ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na utumishi wa umma unaotenda haki na wenye kuwajibika kwa umma.
Aidha, amebainisha kuwa, taasisi za umma zinapokuwa na malalamiko mengi ya watumishi ni ishara kuwa watendaji wa ofisi hizo hawafanyi kazi ipasavyo hata kama lalamiko liko ndani ya uwezo wao. Hivyo, kitendo cha kupeleka malalamiko hayo katika ngazi za juu kwa utatuzi ni dhihaka kwa utawala.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi amesema Maofisa hao ni washauri wakuu wa Maafisa Masuuli katika taasisi zao, hivyo wanatakiwa kutoa ushauri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili kuepuka kuumiza watumishi.
Bw. Mkomi amewasihi maofisa hao kuhakikisha wanatatua matatizo ya watumishi wa umma kwa kuwasikiliza na wakati mwingine kuwaonya kwanza kuliko kuwafukuza katika utumishi wa umma.
Awali, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Hilda Kabissa amesema kikao kazi hiki kimelenga kuwajengea uwezo Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria katika kutekeleza Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Amesema, anaamini mada zilizowasilishwa zimeeleka kwa vizuri na washiriki wameahidi kuzifanyia kazi mafunzo haya kwa umahiri mkubwa sana na kuhakikisha wanahimiza haki na wajibu kwa watumishi wa umma.
Ameongeza kuwa maofisa hao pamoja na mambo mengine wamepitishwa katika masuala ya maslahi ya watumishi, uzingatiaji wa maadili mahala pa kazi, mifumo ya TEHAMA Serikalini, kutambua mifumo ya upimaji wa utendaji kazi Serikalini, utaratibu wa kuendesha mashauri ya kinidhamu katika utumishi wa umma.