Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC),akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani na kumnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Kimbiji Ndg. Maimuna Mwinyipingu Yusufu iliyopo wilayani Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC),akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Kimbiji Ndg. Maimuna Mwinyipingu Yusufu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
…..
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameeleza jinsi Viongozi Wanawake ni wachapakazi,wazalendo na waadilifu wanapopewa nafasi mbalimbali za kiuongozi katika jamii na kuleta maendeleo.
Chatanda ameeleza hayo jana jumapili Machi 17, 2024 wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani na kumnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Kimbiji Ndg. Maimuna Mwinyipingu Yusufu iliyopo wilayani Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam.
“Hamkukosea kumpa Maimuna katika kura za maoni,Viongozi wanawake ni wachapakazi,wazalendo na waadilifu,ni waleta maendeleo.Mfano ni Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan utendaji bora wa kazi zake unadhihirisha ubora wa viongozi wanawake”Alisema Mwenyekiti Chatanda na kuongeza
“Mtakapomchagua Ndg. Maimuna kuwa Diwani wa Kata ya Kimbiji atashirikiana na viongozi wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuleta maendeleo katika Kata ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kama inavyotekelezwa katika maeneo yote ya nchi.”
Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata ya Kimbiji unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 20 Machi 2024.