Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kushoto) akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme (kulia) wakati alipowasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme wakati alipowasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (katikati) wakati alipowasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024. Anayeshuhudia kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme akipokea shada la maua kutoka Mtumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Edna Nkulila, wakati alipowasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024. Anayeshuhudia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme akiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati alipowasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme (kushoto) akizungumza jambo pamoja na Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis (katikati) wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Khamis Hamza Khamis (katikati) na Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Christina Mndeme akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili alipowasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme (wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) (wa tatu kulia) Mhe. Khamis Hamza Khamis na Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga (wa pili kulia) wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu na Mkurugenzi wa Tathimini na Ufuatiliaji, Bw. Sigsbert Kavishe wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Machi 13, 2024.
(PICHA NA MPIGAPICHA WETU)
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme ameahidi kushirikiana na Viongozi pamoja na Watendaji wa ofisi hiyo kusimamia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanawake wa Tanzania wanahama kutoka katika nishati isiyo safi ya kupikia kwenda katika nishati safi na salama ifikapo mwaka 2030.
Bi. Mndeme amesema hayo wakati alipojitambulisha kwa Viongozi wa Ofisi ya Makamu wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis na Katibu Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo Machi 13, 2024 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Amesema nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kimkakati inayolenga Mwanamke wa Kitanzania na kupewa kipaumbele na Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi na rahisi ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ikiwemo kupunguza gharama ya ununuzi wa vifaa.
“Mwishoni mwa wiki hii wakati tukisherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, tumeshuhudia kongamano kubwa la masuala ya nishati safi ya kupikia na maelekezo na mahsusi ya viongozi yametolewa, hili ni agizo ambalo halina budi kusimamiwa” amesema Bi. Mndeme.
Aidha ameeleza kuwa atatumia uzoefu, juhudi na maarifa katika kusimamia majukumu ya ofisi yake na kuahidi ushirikiano baina yake na Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuhakikisha wadau na wananchi wanapata huduma stahili zinazotolewa na ofisi hiyo.
Ameongeza kwa kuzingatia msingi wa majukumu ya ofisi hiyo amejiwekea utaratibu wa kupokea ushauri na mapendekezo ili kuimarisha mfumo wa utendaji kazi na kuleta tija iliyokusudiwa na jamii kwa kuwa na Tanzania yenye Muungano imara, Mazingira safi, salama na endelevu kwa ustawi wa jamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amempongeza Bi. Mndeme kwa uteuzi huo kwani umeongeza nguvu katika safu ya uongozi katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Watanzania.
“Natumai kwa kipindi ulichohudumu ndani ya Serikali utakuwa ni chachu ya mageuzi ya kimkakati utendaji kazi wa ofisi yetu ambayo ina dhamana kubwa ya kudumisha Muungano wetu na sambamba kulinda mazingira” amesema Mhe. Naibu Waziri Khamis.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga ameahidi kutoa ushirikiano kwa Naibu Katibu Mkuu Mndeme katika kutekeleza majukumu ya kiofisi kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza tija kwa Ofisi katika kuwahudumia wananchi.
Kabla ya uteuzi huo, Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na anachukua nafasi ya Dkt. Switbert Mkama aliyemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa sheria.
Hafla ya mapokezi hayo yalihudhuliwa pia na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi, na Watendaji Waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.