ya Nachingwea Mbarouk Balozi amefunga mafunzo ya uongozi, usimamizi na
uendeshaji wa shule za msingi yaliyoendeshwa kwa Walimu Wakuu wa Shule za
Msingi za Mikoa wa Simiyu, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya na Mtwara chini ya
mradi wa BOOST na kusimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)
Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi -ADEM Dkt. Alphonce Amuli ameeleza kuwa
hadi sasa ADEM imeshatoa mafunzo kwa walimu wakuu 4,522 katika awamu ya kwanza
ya mafunzo hayo, na katika awamu hii mafunzo hayo yametolewa kwa Walimu Wakuu
4,620 katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Simiyu, Mbeya, Kigoma na Mtwara
Baadhi ya walimu wakuu walioshiriki mafunzo hayo
Na Fredy Mgunda,Lindi
Katibu Tawala Wilaya
ya Nachingwea Mbarouk Balozi amefunga mafunzo ya uongozi, usimamizi na
uendeshaji wa shule za msingi yaliyoendeshwa kwa Walimu Wakuu wa Shule za
Msingi za Mikoa wa Simiyu, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya na Mtwara chini ya
mradi wa BOOST na kusimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).
Akizungumza katika
ufungaji wa mafunzo hayo, Balozi amewataka walimu hao kwenda kuboresha utendaji
kazi katika vituo vyao vya kazi kwa kihakikisha wanasimamia kikamilifu shughuli
za ufundishaji na ujifunzaji shuleni kwa ubora.
“ADEM imemaliza
kazi yake ya kuendesha mafunzo haya kwa walimu wakuu katika Mikoa sita nchini,
ni wajibu wa Walimu Wakuu mliopatiwa mafunzo haya kwenda kuyatumia katika
utendaji wenu wa kila siku ili kufikia adhma ya Serikali ya kuboresha elimumsingi
nchini” Amesema. Balozi
Balozi aliwataka
Walimu Wakuu kuongoza shule kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma
na kusimamia miradi ya elimu wanayotakiwa kusimamia kwa ufanisi kwani kupitia
mafunzo hayo wamejengewa uwezo kuhusu usimamizi wa rasilimali za shule hususani
fedha na miradi ya ujenzi inayotekelezwa shuleni.
Balozi alimalizia kwa
kuupongeza uongozi wa ADEM kwa kuendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa na
kuwataka kuendelea kuendesha mafunzo hayo kwa umahiri huo huo katika Mikoa iliyobaki.
Nae Makamu Mkuu wa
Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi -ADEM Dkt. Alphonce Amuli ameeleza kuwa
hadi sasa ADEM imeshatoa mafunzo kwa walimu wakuu 4,522 katika awamu ya kwanza
ya mafunzo hayo, na katika awamu hii mafunzo hayo yametolewa kwa Walimu Wakuu
4,620 katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Simiyu, Mbeya, Kigoma na Mtwara
kuanzia februari 15 hadi machi 13, 2024.
Dkt. Amuli aliwataka
walimu kutumia mafunzo hayo katika kuboresha utendaji na usimamizi wa shule ili
kuleta tija na thamani ya fedha iliyotumika kuyaendesha ionekane.
alisema kuwa Lengo la
mafunzo ni kumjengea uwezo Mwalimu Mkuu kutekeleza majukumu yake ya kusimamia
shule hususani katika kuhakikisha shughuli za shule zinafanyika kwa ubora na
ufanisi unaotakiwa. Mwalimu Mkuu ni mtendaji muhimu katika ngazi ya shule.
Dkt. Amuli alisema
kuwa baada ya mafunzo hayo, washiriki watafuatiliwa na kupimwa katika maeneo
yote waliyowezeshwa,Miongoni mwa viashiria vya utekelezaji wa mafunzo kwa
Mwalimu Mkuu ni pamoja na uwepo wa taarifa zifuatazo,Mpango wa Jumla wa
Maendeleo ya Shule,Mpango wa kushughulikia malalamiko kwa Watumishi, wanafunzi
na jamii,Mpango wa Motisha kwa wafanyakazi na wanafunzi,Miundombinu bora ya
shule,Matokeo chanya ya ujifunzaji na ufundishaji shuleni.