Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa taarifa kuwa mtuhumiwa Dainess Paul Mwashambo [30] mkazi wa Kijiji cha Mashese aliyekuwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya amefariki dunia tarehe 09 Machi, 2024 majira ya saa 10:15 jioni.
Awali Machi 05, 2024 mtuhumiwa Dainess Paul Mwashambo [30] akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese – Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya “Pare Force” watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao na kisha na yeye alikunywa sumu hiyo iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.
Mtuhumiwa aliendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo lakini tarehe 09 Machi, 2024 alifariki duniani.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.