NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Msaidizi Uendelezaji Sera Elimu Msingi Bw.Victor George,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MTHIBITI Ubora wa Shule Kanda ya Kati Bi.Nanzia Abdu Mahuna,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Elimu TAMISEMI Dkt.Emmanuel Shindika,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wadau wa Elimu wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wanafunzi wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MRATIBU wa Lishe kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Bi.Grace Shileringo,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
NAIBU Mkurugenzi wa Shirika la Global Communities wanaotekeleza mradi wa Pamoja Tuwasilishe, Vick Macha,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya chakula shuleni ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wanafunzi.
Hayo yamesemwa leo Machi 1,2024 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula,wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku.
Dkt.Rwezimula amesema wanatambua kwamba utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni ni suala mtambuka linalohitaji ushiriki wa sekta na wadau mbalimbali.
“Nitumie fursa hii kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, makampuni binafsi pamoja na vyombo vya Habari, kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha kuhusu umuhimu wa huduma hii shuleni.”amesema Dkt.Rwezimula
Aidha,amewaomba wadau wa elimu na lishe kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali yetu katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kushiriki kikamilifu kuhamasisha na kuchangia huduma ya chakula shuleni.
“Wizara ya Elimu,itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.”amesema Dkt.Rwezimula
Hata hivyo ameipongeza OR-TAMISEMI kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Wizara ikiwemo mwongozo wa lishe shuleni.
“Nimeelezwa kuwa tayari OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la WFP imeandaa mpango wa utekelezaji wa Mwongozo tajwa ili kuwezesha utekelezaji fanisi wa afua za lishe shuleni.”amesema
Amesema kuwa Mpango huo ambao ulizinduliwa Mwezi Novemba, 2023, utatumiwa na wadau wa lishe katika kuhamasisha wazazi/walezi kuendelea kuchangia chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni.
Hata hivyp ameeleza kuwa maadhimisho hayo ni ya kwanza kufanyika nchini na ni kwa mstakabali wa wanafunzi wanaosoma shule za awali, msingi na sekondari.
“Lengo ni kuhamasisha jamii, wadau na serikali kuweka mikakati ya kutekeleza afua za lishe shuleni , yapo madhara makubwa ya kukosekana kwa chakula kuwa ni njaa, usikivu, utoro wa rejereja na kukatisha masomo,”amesema Dkt.Rwezimula
Awali Mratibu wa Lishe kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Bi.Grace Shileringo ameipongeza serikali kwa kuendelea kuchagiza masuala ya Lishe na kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha jamii nzima inashirika katika kuchangia chakula ili watoto wapate lishe bora shuleni.
“kwa sasa wazazi wengi wamehamasika kuchangia na kushirikiana na shule kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni wakiamini kuwa kufanya hivyo itawasaidia wanafunzi kuwa na utulivu wakati wakiwa Darasani.”amesema Bi.Grace
Kwa upande Wake Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Global Communities wanaotekeleza mradi wa Pamoja Tuwasilishe,Bi. Vick Macha, amesema kuwa wamekuwa wakitekeleza kwa miaka 10 utoaji chakula shuleni kwa mikoa ya Dodoma na Mara.
“Tumekuwa wadau wa muhimu sana katika eneo hili la lishe mashuleni na tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya elimu,sayansi na Teknoliojia na OR-TAMISEMI kwa kuendelea kushirikiana nasi katika eneo hili muhimu la Lishe mashuleni ili kuendelea kuwasaidia wanafunzi wetu wawapo shuleni,”amesema Bi.Vicky
Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni (Africa Day of School Feeding) yamekuwa yakiadhimishwa kila mwaka barani Afrika ambapo mwaka huu kikanda yanaadhimishwa nchini Burundi ikibebwa na Kaulimbiu isemayo “Uwekezaji katika huduma ya chakula na lishe shuleni huchangia matokeo bora ya kielimu”