Na Maelezo Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlakaya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yussuf amesema Serikali imeamua kuweka eneo jengine jipya la kupokelea mafuta litakaloendena na ukuaji wa uchumi wa Kisiwa cha Pemba.
Ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa kituo kikuu cha kupokelea mafuta Wesha kupitia (OR) Fedha na Mipango chini ya Ofisi ya Msajili wa hazina, ZURA na Kampuni ya GPP Tanzania Ltd.
Amesema kwa hatua ya awali wataanza na ujenzi wa hifadhi ya mafuta lita milioni tano, ambapo lita milioni mbili na nusu zitakua mafuta ya petrol,lita milioni mbili diseli na lita laki tano mafuta ya taa.
Kwa upande wake, Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Ibrahim Sanya amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia miundombinu iliyopo sasa kuchakaa na kutokukidhi mahitaji ya kisiwa hicho.
Nae, Katibu Mtendaji Kampuni ya GPP Tanzania Ltd Badali Soud ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuimarisha miundombinu ikiwemo miradi mingi ya maendeleo inayoendelea kujengwa kisiwani humo.