MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi shirika la viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Shirika hilo (Viwango House) leo Februari 28,2024 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Dkt.Athuman Yusuf Ngenya,akielezea jinsi watakavyomsimamia Mkandarasi ili aweze kukamilisha kwa wakati.
Na.Nestory James-DODOMA
MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi shirika la viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande amemtaka mkandarasi anayejenga mradi wa ujenzi Jengo la makao makuu ya Shirika hilo (Viwango House) kuongeza nguvu kazi pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha jengo hilo kama mkataba unavyoeleza.
Prof.Chande ameyasema hayo leo Februari 28,2024 jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Amesema Bodi haijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi huo hivyo tunaomba ufanye kazi usiku na mchana ili jengo liweze kukamilisha hivyo ongeza nguvu kazi.
“Sisi kama bodi hatujaridhishwa kasi ya Mkandarasi katika kukamilisha ujenzi wa ofisi hii Mradi huu unatekelewa wa gharama ya shilingi bilioni 24 tumemtaka ahakikishe anaongeza nguvu kazi ili jengo hili likamilike kwa haraka maana tunataka kuhamia Dodoma kama maagizo ya serikali yanavyotutaka”. Amesema Prof Chande Aidha amesema .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Dkt.Athuman Yusuf Ngenya amesema wanajipanga kumsimamia mkandarasi ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati
“Tumekija hapa kanda yakati kufatilia huu mradi na tukitoka hapa tutaelekea kanda ya ziwa na kanda nyingine na kama mnavyofahamu hapa ni makao makuu ya nchi kwahiyo lazima shughuli za TBS Ziwepo kwa uwakika hivyo ni lazima ujenzi huu Uende kwa haraka” amesema Dkt.Ngenya
Mradi wa ujenzi jengo la Shirika la viwango Tanzania TBS utagalimu takribani Bilion 24 ambapo mpaka sasa mkandarasi amekwishalipwa shilingi Bilioni 8 ambapo ujenzi ulianza mwezi wa tatu mwaka 2022 na ulipaswa kukamilika mwezi wa tatu mwaka huu.