Aidha Kamishna Jenerali Lyimo,amesema kundi hilo la wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo kama litapatiwa elimu na kutambua madhara ya rushwa na dawa za kulevya tutakuwa na taifa lenye utulivu na uchumi imara.
“Rushwa na dawa za kulevya madhara yake yanafanana hivyo basi kama waelimishaji umma mtajikita kwenye utaojai wa elimu kwa umma mtasaidia taifa kuwa na watu wasiojihusha na rushwa au dawa za kulevya”amesema Kamishna Jenerali Lyimo
Kamishna Jenerali Lyimo,amesema kuwa kupitia muunganiko wetu na klabu ambazo tayari tumeshanzianzisha huko mashuleni itasaidia kuwafikia kwa uharaka zaidi watu katika ngazi za mitaa hadi huko kwenye Halmashauri kwani wanafunzi wengi wanatokea huko.
Hata hivyo amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanaathari kijamii na kiuchumi kwani yanachanagia kuathiri nguvu kazi ya taifa na kuondoa utulivu wa nchi.
“Kama taifa litakuwa halina utulivu hata wawekezaji watashindwa kuja kuwekeza kutokana na matukio ya kiharifu yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya”amesema
Kwa upande wake Naibu Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bi. Neema Mwakalyelye, amesema katika mafunzo hayo ya siku tatu washiriki wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo tatizo la dawa za kulevya nchini.
“Pia wamejengewa uwezo wa namna ya kupambana na dawa za kulevya na vita ya rushwa kwani biashara ya dawa za kulevya kwa sehemu kubwa inahusisha na rushwa”amesema Mwakalyelye