Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Iringa mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa moja linaloendelea kujengwa mkoani humo.
Na.Lusungu Helela- Iringa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kudhibiti mianya ya rushwa katika fedha za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali nchini ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.
Ametoa kauli hiyo leo alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la ofisi za TAKUKURU mkoani Iringa ambapo amemtaka Mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ifikapo mwezi Juni mwaka huu kama ilivyopangwa ili watumishi wa taasisi hiyo waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri.
“Tukawe watu wa kupekenyua pekenyua kwenye miradi hii inayotekelezwa na serikali kwani kuna watu wanatumia vibaya fedha za serikali, penyeni huko kuwadhibiti ili miradi ya maendeleo ikamilike kwa wakati na kwa viwango kama ilivyokusudiwa,” amesisitiza Mhe. Simbachwene
Amefafanua kuwa TAKUKURU inatakiwa kuhakikisha inasimamia na kudhibiti fedha zisipotee lakini bila kuathiri maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini.
“Palipo na shilingi ya Mama Samia waambieni TAKUKURU tupo ila katika kufanya haya tusikwamishe maendeleo” amesisitiza Mhe. Simbachawene.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene ameitaka Taasisi hiyo kuwachukulia hatua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo na hivyo kukwamisha utendaji wa Rais Mhe. Dkt. Samia suluhu Hassan.
“Dhibitini mianya ya kuchezea rasilimali za nchi ikiwemo fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, sehemu ambako fedha imesimamiwa vizuri matokeo mazuri yameonekana, naomba niwasihi kuendelea kuwadhibiti ipasavyo wachezea fedha za maendeleo” amesema Mhe. Simbachawene.
Ameongeza kuwa anataka kuona TAKUKURU ikichukua hatua kwa wale wote wanaokwamisha nia nzuri ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kama hatua hizo hazichukuliwi basi miradi mizuri iliyotekelezwa ionekane ili wananchi wazidi kuwa na imani na serikali yao.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP. Salum Hamduni amesema ujenzi wa jengo hilo la ghorofa moja hadi kukamilika kwake mwezi Juni mwaka huu utagharimu zaidi ya shilingi billioni 1.4.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Halima Dendego ameishukuru serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo huku akiipongeza TAKUKURU kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia fedha za serikali zisipotee kwa maslahi binafsi ya baadhi ya watu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Iringa mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa moja linaloendelea kujengwa mkoani humo.
Sehemu ya muonekano wa Jengo la ghorofa moja la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Iringa linaloendelea kujengwa mkoani humo ambapo linatarajiwa kukamalika mwezi Juni mwaka huu.
Sehemu ya Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Iringa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa moja linaloendelea kujengwa mkoani humo
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Iringa (hawapo pichani) kabla ya Waziri Simbachawene mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa moja linaloendelea kujengwa mkoani humo
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la TAKUKURU Mkoani Iringa kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la TAKUKURU mkoani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wakati akikagua ujenzi wa jengo la TAKUKURU Mkoani Iringa linaloendelea kujengwa Mkoani humo.W
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na baadhi ya Watumishi wa TAKUKURU Mkoani Iringa wakati akikagua ujenzi wa jengo la TAKUKURU Mkoani Iringa linaloendelea kujengwa Mkoani humo.