Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakikagua mashine ya kukamua mafuta ya alizeti katika Kijiji cha Ngh’a,bi walipotembelea na kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mradi wa tanki, kisima cha maji safi pamoja na kitalu nyumba katika Kijiji cha Kazania vilivyokaguliwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira unaotekelezwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Jengo la kliniki ya mifugo likiwa katika hatua ya kukamilika kabla ya kuwekewa vifaa lililotembelewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira unaotekelezwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakikagua mradi wa josho la kuogeshea mifugo katika Kijiji cha Kazania walipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikollojia Vijijini (EBARR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakisikiliza maelekezo kuhusu mradi wa josho la kuogeseha mifugo katika Kijiji cha Kazania walipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakikagua mashine ya kukamua mafuta ya alizeti katika Kijiji cha Ngh’a,bi walipotembelea na kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
…….
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimiza wasimamizi wa miradi kwenye halmashauri kuendelea kuisimamia vyema ili ilete tija kwa wananchi.
Amesema hayo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ilipotembelea na kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikoklojia Vijijini (EBARR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mhe. Khamis amesema kuwa ni muhimu kwa wasimamizi hao kusimamia vyema fedha zinazoletwa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo, hivyo kuleta matokeo tarajiwa na kuwanufaisha walengwa.
Pia, amewataka wananchi walionufaika na miradi hiyo kuitunza ili idumu hatua itakayosaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoyakabili meneo kadhaa nchini na duniani kwa ujumla.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Anna Lupembe ametoa pongezi kwa Ofisi ya Makamu ya Rais kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo.
Mhe. Lupembe ametoa wito kwa wananchi kuzungumzia mazuri yanayofanywa na Serikali katika kutekeleza miradi hii mikubwa ambayo imewatatulia changamoto zao.
“Tuipongeze Serikali ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani imewakomboa wananchi kwa kuwatua wanawake ndoo kichwani na kuwawezesha kujipatia kipato kupitia mradi huu wa maji na kitaku nyumba tukichotembelea,” amesema.
Miradi ilitembelewa na Kamati ni pamoja na mashine ya kukamua mafuta ya alizeti na kliniki ya mifugo katika Kijiji cha Ngh’ambi, josho la kuogeshea mifugo na kisima pamoja na kitaku nyumba katika Kijiji cha Kazania.
Mradi wa EBARR unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu (Shinyanga), Mvomero (Morogoro), Mpwapwa (Dodoma), Simanjiro (Manyara) kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Tanzania Zanzibar unatekelezwa katika Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kupitia mradi huu wananchi wanajengewa uwezo wa kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha uwezo wao wa uvumilivu na uwezo wa mifumo ikolojia inayowazunguka kusaidia katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.