KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Prof . Jamal Katundu ( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya EWURA Kanda ya Magharibi mjini Tabora leo 19 Februari 2024. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilile Mwainyekule, na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt John Rogath Mboya. Wanaoshuhudia ni Wajumbe wa Bodi ya EWURA, wakiongozwa na Mwenyekiti Prof Mark Mwandosya ( wa pili kutoka kushoto) na Meneja wa Kanda, wa kwanza kuli Mha. Walter Christopher.
Na.Mwandishi Wetu-TABORA
* Asisitiza Uadilifu, Uchapakazi na Uwajibikaji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Jamal Katundu, leo 19 Februari 2024 kwa niaba ya Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Hamidu Aweso, amezindua Ofisi ya EWURA Kanda ya Mgharibi itakayotoa huduma za udhibiti wa huduma za nishati na maji katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kigoma na Katavi.
Prof. Katundu pia, amefungua kikao cha pili cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa EWURA na kuwasisitiza kuwa waadilifu, kuongeza kasi ya usimamizi wa huduma; kuhakikisha ubora na kulinda maslahi ya walaji, kuwajali wateja wake kama wafalme kwa kuongeza maarifa katika kutatua migogoro kati ya wateja na watoa huduma.
“ Itambulike kwamba uadilifu ni nguzo kubwa katika kufanikisha majukumu yenu ya udhibiti, ninawapongeza sana kwa kuwa mmeiweka kama tunu yenu ya kwanza ya utendaji wenu ninawaomba muendelee kuizingatia”
Pia, ameikumbusha Bodi na Menejimenti ya EWURA kusimamia ustawi wa wafanyakazi kwa kuendelea kuboresha maslahi yao, kuwapatia fursa ya kufanya mazoezi na kushiriki michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao.
Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa EWURA ipo mbioni kuanzisha kituo fanisi cha taarifa zote za udhibiti nchini ili kukidhi dira ya kuwa taasisi ya kimataifa ya udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dokta John Rogath Mboya ameishukuru EWURA kwa kuanzisha Ofisi ya Kanda mkoani Tabora na kuihakikishia Mamlaka ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Baadhi ya Wakurugenzi na Mamemeja wa EWURA wakimsubiri mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya EWURA Kanda ya Magharibi leo 19 Februari 2024.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Prof . Jamal Katundu ( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya EWURA Kanda ya Magharibi mjini Tabora leo 19 Februari 2024. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilile Mwainyekule, na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt John Rogath Mboya. Wanaoshuhudia ni Wajumbe wa Bodi ya EWURA, wakiongozwa na Mwenyekiti Prof Mark Mwandosya ( wa pili kutoka kushoto) na Meneja wa Kanda, wa kwanza kuli Mha. Walter Christopher.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Prof . Jamal Katundu ( katikati) Viongozi wa Mkoa wa Tabora,Wajumbe wa Bodi ya EWURA,Viongozi wa Dini Menejimenti ya EWURA wakifurahia baada ya kuzindua Ofisi ya Kanda ya Magharibi Mjini Tabora leo Februari 19,2024.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Prof . Jamal Katundu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya EWURA mara baada ya kuzindua Ofisi ya EWURA Kanda ya Magaharibi mjini Tabora leo 19 Februari 2024.