Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Catherine Bamwenzaki akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa Sheria waliopo Mpaka wa Sirari Mkoani Mara leo( Jumamosi Februari 17, 2024) wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza tarehe 17 hadi 18 Februari, 2024 yanayolenga kujenga uelewa kuhusu kudhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Catherine Bamwenzaki akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa Sheria waliopo Mpaka wa Sirari Mkoani Mara leo( Jumamosi Februari 17, 2024) wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza tarehe 17 hadi 18 Februari, 2024 yanayolenga kujenga uelewa kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni. Katikati ni Meneja Msaidizi wa Forodha, Mkoa wa Mara Bw. Said Hemed na Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mhandisi George Ngoso
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozone wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozone wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozone wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara
Mkufunzi kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mbegani, Bagamoyo Pwani akifuatilia wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara. Wengine pichani ni Maafisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Jeniva Olengeile na Bi. AnnaMaria Gerome.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Catherine Bamwenzaki (katikati mstari wa mbele) pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo (wa pili kulia) pamoja na washiriki mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo leo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Catherine Bamwenzaki (katikati mstari wa mbele) pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo (wa pili kulia) pamoja na washiriki mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni leo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Dustan Shimbo akizungumza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Kanuni za Kudhibiti Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni) za mwaka 2022 kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa Sheria Mipakani kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni leo Jumamosi tarehe 17-18 Februari, 2024 katika Mpaka wa Sirari Mkoani Mara.
Mkaguzi wa Madawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Bw. Frank Mhini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa Sheria waliopo Mpaka wa Sirari Mkoani Mara leo( Jumamosi Februari 17, 2024) wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza tarehe 17 hadi 18 Februari, 2024 yanayolenga kujenga uelewa kuhusu kudhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Na Mwandishi Wetu,-OMR- SIRARI,
SERIKALI imewataka maafisa forodha na wasimamizi wa sheria mipakani kuendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti wa kemikali zinazodhibitiwa zinazochangia kumong’onyoa tabaka la ozoni kunakochangia ongezeko la joto duniani na husababisha mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, Mhandisi Catherine Bamwenzaki wakati akifungua Mafunzo ya Maofisa Forodha na Wasimamizi wa Sheria mipakani kuhusu udhibiti wa uingizaji wa kemikali zinazodhibitiwa chini ya Itifaki ya Montreal leo Jumamosi Februari 17, 2023 katika ukumbi wa Mpaka wa Sirari, Mkoani Mara.
Mitawi ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wa kueneza elimu ya ozoni kwa wadau wengine ili kuongeza uelewa na juhudi za pamoja katika kuhifadhi tabaka la ozoni, na hivyo kuokoa maisha ya binadamu, wanyama na viumbe hai mbalimbali duniani.
“Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni ni kemikali/gesi zinazotumika katika majokofu na viyoyozi mbalimbali, vifaa vya kuzimia moto, usafishaji chuma, utengenezaji magodoro. Ni wajibu wetu kama Maafisa wa Serikali katika maeneo ya mipaka tusimamie vyema sheria ili kujikinga na madhara ya kemikali hizi” amesema Mitawi.
Kwa mujibu wa Mitawi ametaja madhara ya uharibifu wa tabaka la ozone ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo saratani ya ngozi, mtoto wa jicho, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi na kujikunja kwa ngozi na kuathirika kwa ukuaji wa mimea.
Ameongeza kuwa kutokana na madhara ya kemikali hizo, Serikali imekuwa ikiendesha mafunzo kwa wasimamizi wa sheria na maafisa wa forodha mipakani kwa kuzingatia kuwa ndio wahusika wakuu katika kudhibiti uingizaji wa bidhaa mbalimbali mipakani zikiwemo kemikali hizo katika maeneo yao ya kazi.
Akiwasilisha Mada kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Kanuni za Kudhibiti Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni) za mwaka 2022, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo amesema katika kutekeleza Itifaki ya Montreal, Serikali imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali iliwemo Mpango wa Kuondosha Kemikali Zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni Jamii ya Hydrochlorofluorocarbons (HCFCs) ifikapo mwaka 2030.
Ameongeza kuwa Serikali ipo katika maandalizi ya Mpango wa utekelezaji wa Marekebisho ya Kigali ya kupunguza matumizi ya kemikali jamii ya hidrofluorokaboni ambapo mojawapo ya shughuli zinazotelekezwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Serikali walioko mipakani ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za mwaka 2022.
Kwa upande wake, Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mhandisi George Ngoso amesema suala udhibiti wa kemikali na vifaa vya kemikali linahitaji nguvu ya pamoja vaina ya wadau waliopo katika mnyororo wa thamani ili kulinda afya za binadamu na mazingira.
Mhandisi Ngoso amesema ni wajibu wa mawakala wa forodha waliopo mipakani kujifunza teknolojia mpya ya ukaguzi wa mizigo ikiwemo bidhaa za kemikali kuendelea na usimamizi na udhibiti wa kemikali zinazodhibitiwa kwa kuzingatia ukomo wa matumizi wa kemikali hizo.
“Mnapaswa kuwa wazalendo na kutanguliza maslahi ya taifa na jamii inayowazunguka, madhara ya uingizaji wa bidhaa hizi unaweza kuleta athati kuwa kwa afya za binadamu na mazingira, hivyo tunapaswa kuhakikisha kuwa tunadhibiti kemikali hizi kutoweza kuingia katika jamii yetu” amesema Ngoso.
Tanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Vienna unaohusu hifadhi ya Tabaka la Ozoni na Itifaki ya Montreal kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni ambapo Mkataba huo iliridhiwa na nchi mwaka 1993.
Katika mafunzo hayo washiriki hao walielimishwa kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Kanuni za Kudhibiti Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni) za mwaka 2022, Sayansi ya Ozoni na athari zitokanazo na uharibifu wa tabaka la ozoni, Matumizi ya Mitambo ya Kutambua Gesi zinazoharibu Tabaka la Ozoni.
Jumla ya Mawakala wa forodha na Wasimamizi wa Sheria 25 waliopo katika Mpaka wa Sirari, Mkoani Mara walishiriki mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza tarehe 17 hadi 18, 2024 na kuandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.