Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi lilofanyika tarehe 16Februari,2024 Jijini Dodoma.
……………..
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania -TACAIDS Dkt Jerome Kamwela, ameongoza kikao cha Baraza la wafanyakazi la Tume hiyo, kilichofanyika tarehe 16Februari,2024 jijini Dodoma, ambapo alichukua nafasi hiyo kuongoza uchaguzi wa upatikanaji wa Katibu na Katibu msaidizi.
Katika Uchaguzi huo majina pendekezwa yalikuwa ni mawili ambayo ni Bi.Jaqline Lema na Dkt Hassan Ishabairu, baada ya kura kupigwa, Dkt Hassani Ishabairu alishinda kuwa Katibu wa Baraza la wafanya kazi la Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania -TACAIDS.
Baada ya uchaguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela, aliwataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TACAIDS kushiriki kikamilifu kwa kuchangia na kujadili hoja muhimu zitakazopelekea uboreshaji na ufanisi wa majukumu ya Tume.
Amesisitiza kuwa kikao hiki ni muhimu kwa taasisi yetu hivyo kila mtumishi azungumze bila hofu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika maeneo yetu na kuleta umoja, mshikamano na upendo katika maeneo ya kazi.
Kupitia kikao hicho wafanyakazi bora tisa wa TACAIDS wa mwaka 2023 wamepatiwa zawadi kwa mujibu wa taratibu za chama cha wafanyakazi.
Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti Bw. Godfrey Godwin aliwasilisha Mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2022/23, Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2023/24 kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Disemba 2023 na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Tume ya mwaka wa Fedha 2024/25.
Wakuu wa Idara na vitengo wamewasilisha mipango ya bajeti ya Idara zao ambayo wameipanga kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Tume mwaka wa fedha 2024/25 ambapo wajumbe walipata nafasi ya kujadili na kupitisha mipango hiyo.
Baada ya Mawasilisho hayo Baraza la wafanyakazi limepitisha bajeti hiyo ya mwaka 2024/25 kwa hatua nyingine Zaidi, Mwakilishi wa TUGHE Taifa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji TUGHE Taifa Dr. Allan Masanja amesema TACAIDS imefanya kazi nzuri kupitia taarifa zake ilizowasilisha na amewapongeza kwa ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Amewataka kutekeleza bajeti kwa ufanisi ambayo wameiandaa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwani pamoja na kazi kubwa ambayo inatekelezwa na Tume hiyo kwa ufanisi bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwakuwa jamii kubwa bado inahitaji huduma kutoka TACAIDS.
“Tunawapongeza mnavyojitahidi kuhakikisha Taifa letu linapata elimu ya kujikinga na maambuzi ya VVU lakini bado kuna jamii kubwa ambayo bado inawahitaji kupata huduma yenu,hasa sehemu za vyuo na maeneo yenye uhatarishi wa kupata maambukizi ya vvu”alisema Allan Masanja
Aidha amewataka watendaji wa TACAIDS kudumisha upendo na nidhamu mahala pa kazi na kuchapa kazi ili malengo yaliyowekwa kufikia asilmia 100, ikiwa ni pamoja na kutoruhusu vishawishi vya rushwa kwani ni adui wa haki .
Katibu wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Dodoma (TUGHE) Bw. Samweli Nyungwa amewapongeza wafanyakazi wote waliopatiwa vyeti na zawadi za wafanyakazi bora na kuwataka wahakikishe zawadi hizo wanaendelea kuzitendea haki kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi lilofanyika tarehe 16Februari,2024 Jijini Dodoma.
Katibu wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Dodoma (TUGHE) Bw. Samweli Nyungwa akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa baraza la wafanyakazi kuwa lipo kwa mujibu wa sheria ambalo ni agizo la Rais No.1 la mwaka 1970 ambalo kazi zake ni pamoja na kuishauri serikali katika shuhghuli zake na kuhakikisha watumishi wa serikali wanashirkikishwa kwenye shughuli za kiserikali.
Mkurugenzi wa fedha na Utawala Bw.Yasin Abas akifafanua maswauala ya Kiutumishi baada ya kuwasilisha Bajeti ya Idara yake.
Mmoja wa washindi wa wafanyakazi bora Bw. Geofrey Mabu akikabidhiwa Cheti na fedha Taslim, anayempongeza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela, aliyesimama katikati ni Mwakilishi wa TUGHE Taifa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji TUGHE Taifa Dr. Allan Masanja na Mwisho kabisa Naibu Katibu wa Baraza la wafanyakazi TACAIDS Bi Jacqline Lema.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti Bw. Godfrey Godwin aliwasilisha Mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2022/23, Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2023/24 kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Disemba 2023 na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Tume ya mwaka wa Fedha 2024/25.
Mmoja wa watumishi Bw. Enrico Kawanga akichangia namna Tume inaweza kutumia maandiko ya kiushawishi kusaidia upatikanaji wa vyanzo vya fedha za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI –ATF, baada ya wasilisho la bajeti ya Idara ya Fedha na Utawala.
Baadhi ya watumishi walioshiriki kwenye kikao cha Baraza la wafanyakazi la TACAIDS kilichofanyika tarehe 16Februari,2024 jijini Dodoma.