NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Dkt.Wilson Mahera, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati  wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

MGANGA Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange (hayupo pichani), akizungumza wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

MWENYEKITI  wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara you Dkt. Florence Hilari,akizungumza kwa niaba yao wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange,amesema serikali haitamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atashindwa kusimamia usalama wa vifaa tiba vinavyopelekwa kwa ajili ya  kuboresha huduma za afya nchini.

Dkt. Dugange ametoa  maelekezo hayo leo  Februari 13,2024 Jijini Dodoma akizungumza na Waganga wafawidhi wakati  kakifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi”.

“Ni Jukumu lenu Waganga wafawidhi kuhakikisha  mnasimamia kwa ufanisi mkubwa vifaa tiba na kuvitumia kwa matumizi sahihi na si vinginevyo” amesema Dkt. Dugange 
Pia amewataka kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuleta thamani ya uwekezaji wa Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya nchini.
Aidha Dkt.Dugange amewataka waganga hao kuimarisha ushirikiano wao na watumishi wanao waongoza ili kuleta ubora wa huduma katika kuwahudumia wananchi.
“Kama wananchi watafika mahali hawaoni tofauti ya ukiwepo na usiwepo basi wewe kitaaluma ni mfu maana taaluma yako haigusi maisha ya watu”. amesema 
Hata hivyo amewataka kutenga bajeti katika kila mwaka wa fedha kwa ajili ya kununua mafuta kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
“Tuzingatie utoaji wa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum hasa Albino, tengeni bajeti ya mahitaji maalum kulingana na mahitai yao, utengaji wa fedha kwaajili ya mafuta maalumu kwa wenye ualibino ni maelekezo ya serikali na ni ya muhimu” alisema Dkt. Dugange
 Amebainisha kuwa katika kipindi Cha miaka mitatu Halmashauri 47 tu zilitenga fedha kwaajili ya mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi, (Albino) hivyo ni vyema katika utoaji wa huduma kuwatambua ili wapate mafuta hayo yatakayowakinga na vitu mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amewataka waganga hao kupita maeneo ya huduma kuangalia wananchi wanavyopata huduma ikiwemo kuangalia muda wanaokaa na kusubiri kupata huduma badala ya kukaa ofisini.

“Nasisitiza daktari, muuguzi, mtaalamu wa maabara na wengine wote piteni mawodini na kufungua majalada ya wagonjwa kuona huduma gani wagonjwa wamepatiwa tangu wamefika hospitali, je wanapata dawa na vipimo vilivyoandikwa, watumishi wapo na kama wanawajibika”. Amesisitiza Dkt. Magembe.

Ameongeza kwa kusema kuwa watumishi wasijifungie maofisini tu, bali watumie ujuzi wao kama viongozi wa vituo kuhakikisha wanatoa Huduma bora kwa wananchi ili kuleta thamani ya uwekezaji wa Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Waganga wafawidhi hao  Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara you Dkt. Florence Hilari ,amesema kuwa watazingatia  maelekezo waliyopewa na kuyafanyia kazi kwa ufanisi na hatimaye kutoa Huduma bora na yenye tija kwa wananchi.