NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Dkt.Wilson Mahera, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
MGANGA Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange (hayupo pichani), akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara you Dkt. Florence Hilari,akizungumza kwa niaba yao wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange,amesema serikali haitamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atashindwa kusimamia usalama wa vifaa tiba vinavyopelekwa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini.
Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo leo Februari 13,2024 Jijini Dodoma akizungumza na Waganga wafawidhi wakati kakifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi”.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amewataka waganga hao kupita maeneo ya huduma kuangalia wananchi wanavyopata huduma ikiwemo kuangalia muda wanaokaa na kusubiri kupata huduma badala ya kukaa ofisini.
“Nasisitiza daktari, muuguzi, mtaalamu wa maabara na wengine wote piteni mawodini na kufungua majalada ya wagonjwa kuona huduma gani wagonjwa wamepatiwa tangu wamefika hospitali, je wanapata dawa na vipimo vilivyoandikwa, watumishi wapo na kama wanawajibika”. Amesisitiza Dkt. Magembe.
Ameongeza kwa kusema kuwa watumishi wasijifungie maofisini tu, bali watumie ujuzi wao kama viongozi wa vituo kuhakikisha wanatoa Huduma bora kwa wananchi ili kuleta thamani ya uwekezaji wa Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya nchini.