MWENYEKITI wa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi,Mhe.Deo Mwanyika akieleza jambo wakati wa semina ya kamati hiyo ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi,Mhe.Deo Mwanyika,akisisitiza jambo wakati wa semina ya kamati hiyo ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Exaudi Kigahe, akichangia jambo wakati wa semina ya kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa,akiwasilisha mada mbalimbali kwa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ikifatilia Semina iliyotolewa kwa kamati hiyo ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
MJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Prof.Sospeter Muhongo,akitoa maoni kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakati wa Semina ya wabunge iliyotolewa kwa Kamati hiyo na Brela iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
MJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Dkt.Medard Kalemani ,akitoa maoni kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakati wa Semina ya wabunge iliyotolewa kwa Kamati hiyo na Brela iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
MKurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Andrew Mkapa,akiwasilisha mada wakati wa Semina ya kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KAMATI ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi imeridhishwa na utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ili kufikia azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Mwanyika ameyasema hayo leo Februari 11,2924 kwenye semina ya kamati hiyo ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Brela iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.
Amesema ni muhimu wabunge kuwa na ufahamu wa taasisi hiyo ili kuisimamia na kufikia azma hiyo kwa kuwa serikali imefanya mageuzi makubwa Brela.
“Mazingira haya mazuri ya biashara ni kwa wawekezaji wa ndani na nje sasa taasisi hii ndio uhai wa mazingira ya biashara, dirisha la kwanza ambalo mwekezaji anakutana nalo ni Brela tunawapongeza sana zile kazia ambazo walikuwa wanapata wawekezaji kwasasa zimepungua sana,”amesema.
Mwanyika amesema hali hiyo itaiweka Tanzania kuwa nchi yenye mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwaasa wajipange kuwalea wafanyabiashara kupitia Maofisa biashara ya Halmashauri.
Naye, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaudi Kigahe, amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa, amesema wamewaeleza wabunge mwelekeo wa wakala huo katika utekelezaji wa majukumu yake na kupokea maoni yao ili kuboresha utendaji kazi wao.
“Tumewaeleza wabunge tunakwenda kupitia sheria ya makampuni ambayo ni ya zamani ili kwenda na wakati katika kuhudumia watanzania na kuhakikisha biashara za watanzania zinakuwa badala ya kuwa na sheria zinazoleta makwazo,”amesema.
Amefafanua kuwa Mwaka 2018 Brela ilianza kutumia mifumo ambayo inawezesha watanzania kusajili kampuni kwa njia ya mtandao.