Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima,akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima,akizungumza mara baada ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bi Fatma Tawfiq ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania, Raphael Charles,akisoma risala wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Kagera – CCM, Mhe.Neema Lugangira,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ulienda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni halfa iliyofanyika leo Februari 10,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima,amezindua kampeni ya ulimzi na usalama wa Mtoto Mtandaoni huku akitoa maagizo mbalimbali ikiwemo wazazi na walezi kuhakikisha mtoto anatumia vifaa vya kieletroniki chini ya uangalizi wao na kutoruhusiwa kulala na simu.
Waziri Gwajima amezindua kampeni hiyo leo Februari 11,2024 jijini Dodoma iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya ushauri kuhusu ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni .
Waziri Gwajima amewataka Wazazi au Walezi kuzingatia hasa kutimiza wajibu wao wa kulea watoto na kufuatilia kwa usahihi matumizi ya vifaa vya kielektroniki hasa wakati wa likizo ili mtoto kuwa salama mtandaoni.
“Wazazi au Walezi wekeni kiwango cha muda wa matumizi ya vifaa vya kieletroniki hasa luninga ili kukwepa janga la urahibu na kutoa muda kwa mtoto kufanya kazi za nyumbani na kujisomea. Hakikisha mtoto anatumia vifaa vya kielektroniki chini ya uangalizi wa karibu ili kutojiingiza katika mitandao ambayo ni hatari kwa usalama wa Mtoto. “amesema Dkt.Gwajima
Aidha amewaasa Wazazi au Walezi, kuwaruhusu watoto kushiriki majukwaa yao yaani Mabaraza ya Watoto shuleni na Madawati ya ulinzi wa Watoto ili kujengeana uwezo wa masuala mbalimbali yanayowahusu.
Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kuhusu utafiti uliyofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF mwaka 2022 kwa watoto wa Tanzania wa umri wa miaka 12 hadi 17 ulioonesha asilimia 67 ya watoto wanatumia mitandao na asilimia 4 ya watoto hao walifanyiwa aina tofauti za ukatili kwenye mitandao ikiwa pamoja na kukutana na wahalifu waliowasiliana nao kupitia mitandao.
Aidha, amesema katika kukabiliana na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao kwa watoto, Wizara kwa kushirikiana na Wadau Kamati hiyo ya Taifa ya Ushauri inayojumuisha Wakurugenzi au Wakurugenzi wasaidizi kutoka Serikalini, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Sekta Binafsi pamoja na kikundi kazi cha wataalamu wa uratibu wa utekelezaji wa mpango kazi wa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa mtandaoni.
Ameongeza pia, kampeni hiyo iliyozinduliwa inahusu kuelimisha watoto wenyewe, wazazi, walimu na jamii kwa ujumla kuhusu kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili ikijumuisha usalama wa mitandaoni ambapo Kaulimbiu itakayoongoza kampeni hii ni Jukumu Letu; Chukua Hatua.
Vilevile Dkt Gwajima amesema ni muhimu wazazi kuwalea watoto kwa kuwaandaa kukabiliana na mazingira ya kidigitali kwani bila kufanya hivyo inakua rahisi kwa watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili kupitia vifaa hivyo.
“Kazi ya Serikali ni kujenga ufahamu kwa wazazi ili waweze kuelewa kuwa katika ulimwengu wakidigitali inabidi tuingie kwa lengo la maendeleo na si kwa ajili ya kukatiliwa
Kwa upande wake Naibu Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandasi Kundo Mathew amesema uwepo wa teknolojia ya akili bandia ni muhimu kwa maendeleo ya mawasiliano katika Taifa lakini unakuja na changamoto zake ambazo zinahitaji umakini wa hali ya juu katika kuzitatua.
“Wizara ya habari na Mawasiliano itaipa kampeni hiii uzito unaostahili ili kutoa matunda sahihi ikiwemo utungaji wa sera kwa kuwashirikisha wadau wote sambamba na kukidhi mahitaji ya kidigitali kwa wakati tulionao “Amesema Mhandis Kundo .
Awali Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania, Raphael Charles amewaasa watoto kuhakikisha wanatumia mitandao ya kijamii kwa kufuata miongozo ya wazazi na walezi ili kuepukana na ukatili unaoendelea katika mitandao ya Jamii.
Hata hivyo amewataka watoto kuhakikisha hawapigi wala kuweka picha za faragha mitandaoni, kutotoa taarifa zao binafsi na familia kwa watu wasiowajua na kutoweka picha za utupu kwakuwa madhara yake ni makubwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Bi. Rosemary Senyamule amesema kuwa mkoa wake ni wahanga wa ukatili kwa watoto ingawa matukio yameonekana kupungua kutoka matukio 4,680 mwaka 2022 hadi matukio 3,676 kwa mwaka 2023.