Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy kuhusu maendeleo ya miradi ya umeme vijijini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza katika Kijiji cha Armanie Wilaya ya Longido mkoani Arusha tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza katika Kijiji cha Armanie Wilaya ya Longido mkoani Arusha tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi la Uzinduzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine kilichopo Kijiji cha Armanie Wilaya ya Longido mkoani Arusha. Tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine kilichopo Kijiji cha Armanie Wilaya ya Longido mkoani Arusha. Tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua Kituo cha Afya Ketumbeine mara baada ya kuzindua kituo hicho tarehe 10 Februari 2024 akiwa ziarani Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akivalishwa vazi la kuwa kiongozi wa jamii ya Kimaasai kutoka kwa Malaighwanani wa kata ya Ketumbeine mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine kilichopo Kijiji cha Armanie Wilaya ya Longido mkoani Arusha. Tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kwaajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa wananchi wa kata ya Ketumbeine Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha mara baada ya kuzindua Kituo cha Afya Ketumbeine kilichopo Kijiji cha Armanie. Tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakimsalimia Mama wa kwanza aliyejifungua kwa njia ya upasuaji katika Kituo cha Afya Ketumbeine wakati wa uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Kijiji Armanie Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha. Tarehe 10 Februari 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Longido mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Afya Ketumbene akiwa ziarani mkoani Arusha tarehe 10 Februari 2024.