KAIMU Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma,Bi.Asha Kwariko wakati ,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 30,2023 jijini Dodoma kuhusu taarifa ya miezi mitatu za kazi za Taasisi hiyo.
Na.Gideon Gregory-DODOMA
KATIKA kipindi cha Miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2023 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma imefuatilia miradi 35 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 21 katika sekta za elimu,ujenzi, afya na Maji.
Hayo yamesemwa leo ,Februari 8,2024 jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Bi.Asha Kwariko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya miezi mitatu za kazi za Taasisi hiyo.
Amesema kuwa wametiliaji wa miradi ya maendeleo 31 yenye thamani zaidi ya Bilioni 21 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Oktoba mpaka Desemba 2023 na kubaini miradi 15 kuwa na mapungufu yenye thamani zaidi ya Bilioni 4.
Kwariko amesema kuwa katika ufuatiliaji huo walio ufanya miradi ya elimu ilikuwa kipaumbele chao kwasababu mwezi Januari walitarajia wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza wengi zaidi wasajiliwe kama ilivyo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule za msingi.
“Katika miradi hii tuliyoifuatilia inatoka katika sekta ya elimu miradi 24, ujenzi miradi 4, afya miradi 3 na maji miradi 4 na hatua tulizo zichukua ni kama ifuatavyo mfano katika Wilaya ya Kondoa tulibaini wizi wa Saruji mifuko 141 umefanywa na baadhi ya wasiimamizi wa mradi na tayari uchunguzi umeanzishwa,” amesema.
Aidha Kwariko ameongeza kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu tumepokea jumla ya malalamiko 165 kati ya hayo 90 hayahusu Rushwa na 75 yalihusu Rushwa.
“Kati ya malalamiko 90 ambayo hayahusu rushwa malalamiko 72 walalamikaji wake walielimishwa, malalamiko Matano yalihamishiwa idara nyingine na malalamiko 13 walalamikaji wake walishauriwa namna bora ya kutatua malalamiko yao,” ameongeza.
Sambamba na hayo ametaja vipaumbele walivyojiwekea katika kuhakikisha wanapambana na Rushwa kuwa wataongeza kasi katika kufanya chambuzi za mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi hasa maeneo ya utoaji huduma kwa wananchi na katika miradi inayogusa wananchi.
“Pia tutaendelea kufanya uchunguzi katika tuhuma zinazoainishwa katika taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, malalamiko ya matumizi mabaya ya Ofisi na mamlaka katika idara ya ardhi katika Jiji la Dodoma na tuhuma zingine kadri zitakavyobainika,”amesema.