Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2024 Jijini Dodoma na kutoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya kuvunjika kwa Kalavati katika barabara ya Kanyinabushwa Mbale “A” iliyoko Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera
Msajili wa Bodi ya Makandarasi (CRB)Mhandisi Rhoben Nkori ,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2024 Jijini Dodoma na kutoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya kuvunjika kwa Kalavati katika barabara ya Kanyinabushwa Mbale “A” iliyoko Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.
Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) pamoja na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) zimetoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya kuvunjika kwa Kalavati katika barabara ya Kanyinabushwa Mbale “A” iliyoko Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ambapo imemtaka Mkandarasi kurudia ujenzi wa Kalvati hilo kwa gharama zake.
Hayo yanajili baada ya maeelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ujenzi Innoncent Bashungwa mnamo Januari 17,2024 yaliyotaka uchunguzi kufanyika juu ya chanzo cha kuvunjika kwa Kalavati hilo.
Akitoa taarifa hiyo leo Februari 8,2024 Jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari Msajili wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi Benard Kavishe mbele ya amesema kuwa mapungufu yaliyosababishwa na uharibifu huo yalisababishwa na mkandarasi hivyo wamemchukulia hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ya Usajili wa Wakandarasi sura ya 35 ya mwaka 2002.
“Tuliunda timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ajali hiyo ambapo timu ilichukua hatua ya kutembelea mradi huo Jnauari 20,2024, kufanya mahojiano na TARURA mkoa wa Kagera,Msimamizi wa mradi na mkandarasi,kupitia nyaraka za mradi huo na kuandaa ripoti ya uchunguzi iliyobainisha chanzo cha kubomoka kwa daraja dogo na kupendekeza hatua stahiki” amesema.
Aidha Mhandisi Kavishe amebainisha kuwa matokeo ya uchunguzi huo kuwa ni kutozingatiwa kwa matakwa ya mkataba ,hasa kutumika kwa malighafi hafifu kinyume na matakwa ya mkataba na kuruhusu kupita kwa vyombo vya moto kabla ya Kalvati kukamilika ujenzi wake.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Rhoben Nkori amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kwa ujumla kuzingatia Sheria ,Kanuni na Miongozo katika utekelezaji wa miradi ili kuepukana na changamoto kama hizo kujirudia.