Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe.Mohamed Mchengerwa,akizungumza leo Februari 7,2024 mara baada ya kuzindua na kushuhudisha majaribio ya ufundishaji mubashara kati ya Shule ya Sekondari Kibaha Mkoa wa Pwani na Shule ya Sekondari Dodoma mkoani Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe.Mohamed Mchengerwa ,amezindua majaribio ya ufundishaji mubashara (Live Teaching) katika Shule ya Sekondari ya Dodoma .
Mhe.Mchengerwa akizungumza mara baada ya kuzindua na kushuhudisha majaribio ya ufundishaji mubashara kati ya Shule ya Sekondari Kibaha Mkoa wa Pwani na Shule ya Sekondari Dodoma mkoani Dodoma.
Amesema kuwa uanzishwaji fundishaji mubashara ni moja ya jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya ugongozi wa Rais Samia, Suluhu Hassan wa kwenda kupunguza uhaba wa walimu nchini.
“Ufundishaji mubashara utasaidia katika kupunguza changamoto ya uhaba wa walimu na kuongeza ufahamu na maarifa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali katika ngazi ya awali, msingi na sekondari.”amesema Mhe.Mchengerwa
Katika hatua nyingine Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuteua shule maalumu ambayo itakuwa nguzo ya kusambaza mifumo hii ya TEHAMA katika shule mbalimbali katika maeneo yao.
“Hakikisheni Kila mkoa lazima Mteue shule kama walivyofanya hapa Dodoma, na kwa Mkoa wa Pwani kama walivyofanya kule Kibaha, na wakuu wa mikoa mingine waanze kuteua shule moja ambayo itakuwa nguzo katika shule mikoa husika kwenda kulitekeleza mara moja.” Amesisitiza
Uzinduo huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule, Wakuu wa Wilaya na Maafisa elimu