Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati alipokwenda kuwafariji wananchi wa Mwamapuli waliopatwa na ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Sehemu ya wananchi wa Mwamapuli akimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Geophrey Pinda.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiteta na mpiga kura wake alipokwenda kuwafariji wananchi waliopatwa na kipindupindu katika eneo la Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda alipokwenda kuwafariji wananchi wa Mwamapuli waliopatwa na ugonjwa wa kipindupindu halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na mpiga kura wake katika eneo la Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akikagua daraja la Mwamapuli wakati alipokwenda kuwafariji wananchi waliopatwa na kipindupindu katika eneo la Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Daraja la Mwamapuli lililopo katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi lilojengwa kwa juhudi za mbunge wa jimbo la Kavuu na na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, MPIMBWE
Wananchi wa jimbo la Kavuu katika eneo la Mwamapuli katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi wamekosa maswali ya kumuuliza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda kutokana na kukamilisha asilimia kubwa ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka 2020.
‘’Hivi mna kero hapa kweli, kuna mtu ana jambo la kumuuliza mbunge kuhusu alichokuwa anasema wakati wa kampeni? na kama yupo anyanyue mkono na aseme’’ alihoji mhe. Pinda.
Hayo yamebainika tarehe 3 Februari 2024 wakati Mbunge wa Jimbo hilo alipokwenda kuwafariji wananchi waliopatwa na ugonjwa wa kipindupindu katika eneo la Mwamapuli halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.
Akiwa katika eneo hilo, Mhe. Pinda amewataka wananchi wa Mwamapuli kufanya kazi kwa bidii na kuweka wazi kuwa inapoelezwa kuwa eneo la Mwamapuli lina changamoto aniatafuta kwa kuwa kazi kubwa ameifanya kulihudumia jimbo la Kavuu.
‘’Wana Mwamapuli ukisema kuna changamoto naitafuta usiku na mchana tulikuwa na changamoto nzito lakini tumeziamua na zimebaki za kawaida tu’’ alisema Mhe. Pinda.
Amewaomba wananchi wa jimbo hilo kutorudi nyuma katika kufanya kazi na kuwaeleza kuwa jimbo la Kavuu lipo juu hususan katika uzalishaji mazao kama vile mahindi na mpunga huku akiwaeleza wana jimnbo hilo kuisikia kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda. Kauli ya kazi iendelee ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan inajidhihirisha kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa miundombinu ya barabara, daraja pamoja na uboreshaji huduma za afya kama vile ujenzi wa vituo vya afya, zahanati sambamba na upatikanaji wa huduma ya maji.
Akigeukia ugonjwa wa kipindupindu uliwapata baadhi ya wananchi wa Mwamapuli, Mhe. Pinda aliwataka wananchi wa eneo hilo kuanza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo kwa kuwa wasafi pamoja na kuhakikisha kila nyumba inakuwa na choo.
‘’Nataka ugonjwa huu uondoke kwa siku moja kwa kuhakikisha mnakuwa wasafi na mnachemsha maji, mnaniahidi kuondoa kipindu pindu ndani ya siku moja?’’ alisema Mhe. Pinda
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda alikuwa jimboni kwake kwa ziara ya siku moja ambapo alifanya shughuli mbalimbali kama vile ukaguzi wa barabara ya kilomita 70 Kibaoni – Sitalike, kukabidhi magari ya wagonjwa pamoja na kuwafariji wananchi waliopatwa na ugonjwa wa kipiundupindu kwenye eneo la Mwamapuli.