MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa (CCM) Jackson Kiswaga amekabidhi la gari la wagonjwa (Ambulance) kwenye kituo Cha Afya Mgama Halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Kiswaga amesema gari hili litarahisisha utoaji huduma kwa wagonjwa pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito.
Amesema lengo la kuomba gari hilo ni kutoa msaada kwa wananchi ili waweze kupelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuitekeleza ahadi yake aliyoiahidi wakati akiomba kura kwa wananchi katika uchaguzi Mkuu 2020 ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Aidha Kiswaga ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupiga hatua katika kuboresha sekta ya Afya nchini vikiwemo vifaa tiba pamoja na watumishi.