Akiwa mkoani Kigoma katika Kata ya Kakonko, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amekutana na kisa cha Mwanamama aliyeachwa na mumewe ambaye ni Meneja wa TANESCO Wilayani Kakonko kwasababu aliyoileza kuwa ni kutopata mtoto.
Katika kuweka hali ya maelewano, Mwenezi Makonda alimuomba Baba huyo mume wa mama huyo kutomfukuza na kumuacha mkewe kwani kuzaa ni jambo la Mpango wa Mungu na yawezekana wakati wa Mungu kwa wao kupata mtoto bado haujafika lakini bado Baba huyo alionesha hali ya ugumu kwa kusema kuwa hana Amani katika maisha yao ya ndoa.
Kutokana na ugumu huo, Mwenezi Makonda aliwaomba Wazee wa Kakonko kupata muda wa kuzngumza na wanandoa hao ilikusudi kuweka maelewano mazuri na kurudiana katika maisha yao ya kawaida.
Vilevile , alimsaidia kiasi cha fedha Tsh. Milioni 5,000,000/= mwanamama huyo ambaye aliomba msaada ili aweze kufanya shughuli itakayomingizia kipato cha kuendesha maisha yake.

