Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania, (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM Kata ya Makuburi wakati akiwasili katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba leo february 2, 2024 kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM ambapo wameadhimisha kwa kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma, kuendesha harambee ya kununua vitabu pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu umuhimu wa kuwa na maadili mema.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba, walimu pamoja na wanachama wa UWT Kata ya Makuburi katika Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika leo February 2, 2024.
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata Makuburi Bi. Severina Minga akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo katika Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika leo February 2, 2024 katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba iliyopo Kata ya Makuburi.
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Kata Makuburi Bi. Severina Minga akizungumza jambo katika Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo akimkabidhi fedha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Yusuf Makamba kwa ajili ya kununua vitabu vya kujisomea wanafunzi wa Shule hiyo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba waliofanya vizuri kitaaluma wakipokea Zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania, (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba waliofanya vizuri kitaaluma wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo pamoja na viongozi wa Kata ya Makuburi.
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo pamoja na viongozi wa Kata ya Makuburi.
Matukio ya picha mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika leo February 2, 2023 katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba iliyopo Kata ya Makuburi.
………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania, (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mwajabu Mbwambo amewataka wazazi kuwa na utamaduni wa kuwafatilia vijana wao wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba kwa ajili kuangalia maendeleo yao jambo ambalo litasaidia kuwa maadili mema na kufanya vizuri kitaalamu.
Akizungumza leo February 2, 2024 Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika katika Kata ya Makuburi, Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mbwambo, amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwa na ushirikiano wa karibu na walimu wa Shule hiyo katika kuhakikisha wanashirikiana kutatua changamoto.
Mhe. Mbwambo amesema kuwa wakati umefika kwa wazazi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kuwaleta wanafunzi wa Shule ili waweze kupiga hatua katika maendeleo ya taalamu.
“Najua kuna wazazi hapa, tusiache jukumu letu la kulea na kuwaacha walimu peke yao, watoto wetu hawataweza kutimiza ndoto za elimu katika maisha yao, naomba mtekeleze majukumu yenu ya msingi na kuwafatilia watoto kila siku” amesema Mhe. Mbwambo.
Amewakumbusha wanafunzi kuacha tabia ambazo sio rafiki zinazoweka kusitisha malengo yao badala yake amewasisitiza umuhimu wa kuweka nguvu ya kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
“Leo tumetoa motisha ya bahasha kwa wanafunzi wezenu waliofanya vizuri kuanzia mwaka wa jana, naitaji mwaka huu zaidi ya wanafunzi 200 wa kidato cha nne mpate daraja la kwanza bila shaka linawezekana” amesema Mhe.
Mhe. Mbwambo.
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata Makuburi Bi. Severina Minga, amesisitiza umuhimu wanafunzi wa Shule hiyo wanaongeza juhudi katika masomo yao.
Bi. Minga amesema kuwa kila mwanafunzi anapaswa kusimamia malengo yake ya kielimu ili aweze kufika ndoto zake na kufanya vizuri.
Amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amefanikiwa kuboresha mazingira ya miundombinu katika Shule hiyo kwa kujenga madarasa ili waweze kusoma katika mazingira rafiki na kufanya vizuri kitaaluma.
“Lengo ni kuwasaidia msome katika mazingira mazingira mazuri pamoja na kuwa maadili mema katika maisha yenu na kupiga hatua” amesema Bi. Minga.
Katika Maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania, (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mbwambo ameungana na UWT Kata ya Makuburi, kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu maadili, kutoa zawadi kwa wanafunzi Bora kitaalamu pamoja kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Yusufu Makamba waweze kujisomea,