Mkurugenzi wa ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Adila Hilal Vuai akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo ya maboresho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 linalotarajiwa kufanyika Februari 05,2024 katika ukumbi wa Golden tulip kiembesamaki,hafla iliyofanyika ofisi ya wizara hiyo Maisara Zanzibar.
Mkurugenzi msaidizi idara ya sera na mipango na kaimu mkurugenzi idara ya diaspora,wizara ya mambo ya nje Justine Kisoka akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari juu ya kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo ya maboresho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 linalotarajiwa kufanyika Februari 05,2024 katika ukumbi wa Golden tulip kiembesamaki,hafla iliyofanyika ofisi ya wizara hiyo Maisara Zanzibar.
Kaimu mkurugenzi ofisi ya mambo ya nje Zanziba r balozi Silima Kombo Haji akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari juu ya kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo ya maboresho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 linalotarajiwa kufanyika Februari 05,2024 katika ukumbi wa Golden tulip kiembesamaki,hafla iliyofanyika ofisi ya wizara hiyo Maisara Zanzibar.
Mwandishi wa habari kituo cha televisheni (ITV) Farouk Kareem akiuliza swali kwa vingozi wa Wizara ya mambo ya nje wakati wakitoa taarifa ya kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo ya maboresho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 linalotarajiwa kufanyika Februari 05,2024 katika ukumbi wa Golden tulip kiembesamaki,hafla iliyofanyika ofisi ya wizara hiyo Maisara Zanzibar.
……………………….
Wananchi wametakiwa kutoa maoni katika mapendekezo ya marekebisho ya Sera Mpya ya mambo ya Nje ili iweze kuendana na wakati uliopo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibar wanaoishi nje ya Nchi Adila Hilal Vuai wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Maisara Mjini Zanzibar.
Amesema Sheria hiyo inahitahija kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya maeneo hivyo iwapo Wananchi watajitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, yatasaidia kuimarika na kuwa bora zaidi kwa Wananchi wa Tanzania.
Amesema Serikali zote mbili zinafahamu umuhimu wa Wananchi kushiriki katika katika maamuzı yanayohusu masuala ya Kitaifa na Kimataifa.
“Ttuhakikishe makundi yote yanashirikishwa katika kutoa maoni yao kabla ya kukamilisha mchakato wa marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje” alisema Mkurugenzi huyo.
Amesema Zanzibar ni Sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo ushiriki wao katika kutoa maoni katika sera hiyo ni muhimu hivyo hakuna budi kushirikiana ili kuweza kutboresha sera hiyo.
Amendelea kwa kusema kuwa upatikanaji wa maoni utawezesha Taifa kunufaika ipasavyo na fursa zitokanazo na ushikiano wa Kimataifa katika utekelezaji wa dhana ya Diplomasia ya Uchumi.
Nae, Kimu Mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji amesema wadau mbalimbali watashirikishwa katika Kongamano hilo, wakiwemo Wanasiasa, Wanataaluma na Watu mashuhuri, Vyama vya Siasa, Taasisi za Dini, Asasi za Kiraia, Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’s) na Wananchi kwa ujumla.
Kongamano hilo litajadili wasilisho la Dhana ya Sera ya mambo ya nje pamoja na Uchumi wa Buluu na Diplomasia ya Uchumi ambapo Mwenyekiti wa Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mhe. Januari Yussuf Makamba ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki na Mwenyekiti mweza ni Mhe. Ali Suleiman Ameir Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu, Zanzibar.
Kongamano hilo la ni mwendelezo wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Sera mpya ya Mambo ya nje baada ya Makongamano yaliyofanyika Mikoa ya Dar-es-Saalam na Arusha ambapo kwa Unguja linatarajiwa tarehe 05 February, 2024 katika Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.