Jeshi la polisi mkoa wa Tabora linamshikilia Hamisi Kulwa (35) mkazi wa kata ya uyogo wilaya ya Urambo kwa tuhuma za kumchinja mke wake mjamzito na kumtoboa tumbo kisha kuwatoa watoto mapacha na kumpika mmoja wapo
Akizungumzia Tukio hilo LEO kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi Richard Abwao mbele ya waandishi wa habari alisema kwamba tukio lililotokea januari 30 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kitongoji cha Isunda kijiji cha milambo kata ya uyogo wilayani urambo mkoani hapa.
Alisema kwamba mtuhumiwa alifanya tukio hilo baada ya kumchinja mkewe na watoto watatu, watoto wawili mapacha waliotumboni na mwingine mmoja aliyekuwa na umri wa miaka miwili kisha kuwazika na kiumbe kimoja alichokitoa tumboni akakipika.
Kamanda Abwao alisema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kwani mwanaume huyo alipokamatwa na kuhojiwa alizungumzia imani hizo za kishirikina
“Tulipomkamata tulipoanza kumuhoji alisema kuwa aliambiwa kuna watu wanamuijia mke wake na watoto wanawapeleka Gambushi kufanya kazi za kichawi kila siku usiku na siku sio nyingi watawaijia na kuwaua ndio maana akaamua awaue yeye mwenyewe” alisema Kamanda Abwao
Alisema kwamba jeshi hilo linaemdelea na upelelezi mara baada ya kukamilika watamfikisha mtuhumi huyo mahakamani kwa mujibu wa sheria
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi mkoani hapa aliwakata wananchi wa kijiji hicho kuachana na imani potofu za kishirikina na kumrejea mungu akisisitiza ndio njia pekee ya kuondokana na mauaji pia kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katani hapo.
Nae Diwani wa kata ya Uyogo, Ntoloki Kazimile alisema ameshangazwa kuona bwana huyo katekeleza kitendo hicho na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutokana na mauaji kuendelea kujitokeza kijijini hapo
Alisema kwamba kitendo hicho ni cha kinyama sana kuwahi kutokea katika wilaya ya urambo na mkoa wa Tabora .