Na.Joctan Agustino-NJOMBE
Akina mama na vijana waliajiriwa katika mashamba ya parachichi,viazi na mazao mengine mkoani Njombe wamelalamikia tabia ya mabosi kuwafanyisha kazi na kisha kuwazulumu fedha licha ya kuamushwa saa kumi alfajiri na kisha kupandishwa kwenye malori kwenda eneo la uzalishaji.
Wakizungumza juu ya changamoto za kufanya kazi ya vibarua ili kupata ujira wa siku katika mashamba mkoani humo akina mama na vijana akiwemo Agnes Bosco wamesema licha ya kuamka alfajiri na kukumbana na vibaka na kisha kusafirishwa na vyombo vyenye usalama mdogo kwenda shambani lakini mabosi wao wamekuwa wakitapeli fedha hivyoo wanaomba serikali na chama kuona namna ya kuwasaidia
“Tunaomba chama kitusaidie hili kuna wakati tunafanya kazi lakini mabosi wetu hawatulipi pesa ,Tunaamka mapema asubuhi tunakimbizana na vibaka njiani na hata usafiri tunaotumia sio mzuri ,alisema AgnesBosco kibarua wa shambani”
Mara baada ya kusikia kero za kundi hilo la vijana na wajasiriamali wanaojitafutia riziki katika mashamba ya mazao ,Ndipo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Njombe Samwel Mgaya akalazimika kuamka saa 10 alfajiri na kwenda kituo cha Nzenge mjini Njombe na kisha kukutana na mamia ya watu wakisubiri usafiri wa lori kwenda shambani ambapo baada ya kusikiliza malalamiko hayo akaahidi kufatilia haki za wote waliotapeliwa.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema amepokea kero ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo na vijana wanaolazimika kuongeza mitaji yao kwa kutafuta ujira wa siku kupitia vibarua vya mashambani na kisha kuahidi kuwasaidia kuanza mchakato wa mikopo ya halmashauri.
Ukiachana na mambo mengine mwenyekiti wa UVCCM imetoa elimu ya lishe na udumavu kwa kundi hilo ambapo akina mama wanasema licha ya kuamka alfajiri lakini hulazimika kuandaa chakula cha watoto kabla ya kutoka ili kulinda afya za watoto wao.
“Huwa tunaamka saa tisa usiku kuandaa chakula cha watoto wa shule na kisha kukiacha na kwamba suala la chakula cha watoto wao linazingatiwa vyema,alisema Salima John”