Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, ametoa agizo la kupiga marufuku matumizi ya simu na mazungumzo ya kibinafsi kwa watumishi wa afya wakati wa kazi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Agizo hilo limekuja baada ya ongezeko la malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu udumavu wa huduma katika vituo vya afya, ambapo watumishi wa afya wamekuwa wakitumia muda mwingi wao kazini kuchati na kufanya mawasiliano ya kibinafsi kupitia simu zao za mkononi badala ya kuzingatia majukumu yao ya kitaalamu.
Profesa Nagu amesisitiza umuhimu wa watumishi wa afya kuzingatia majukumu yao ya kitaalamu wakati wote wa kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na zenye ufanisi kwa wananchi.
Kupitia agizo hili, Mganga Mkuu wa Serikali amejitolea kuhakikisha kuwa huduma za afya zinaboreshwa na kwamba wananchi wanapata huduma bora na za haraka wanapohitaji matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.