Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akimkabidhi mwongozo wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 kwa Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, baada ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania – TOST), katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ni chombo huru chenye jukumu la kupitia na kushughulikia malalamiko yote ya walipakodi kuhusu huduma, masuala ya kiutaratibu na kiutawala yanayoweza kujitokeza katika usimamizi wa sheria za kodi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiitambulisha rasmi Tovuti ya Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania – TOST-www.tos.go.tz), wakati wa Uzinduzi rasmi wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Viongozi wa Wizara ya Fedha, Viongozi wa Dini, Taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na wanahabari.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wakifuatilia kwa umakini halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akibofya kuonesha Nembo rasmi ya taasisi hiyo kama ishara ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, baada ya kumalizika kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, baada ya kumalizia kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Fedha Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba,amezindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) huku akiwataka wauza bidhaa nchini kutoa risiti kwa wanunuaji.
Dkt.Nchemba ameyasema hayo leo Januari 23,2024 jijini Dodoma wakati akizindua Taasisi ya usuluhisho wa malalamiko na taarifa za Kodi.
Dkt.Nchemba amewataka wauza bidhaa kutoa risiti kwa wateja wao hata wanunuaji wanatakiwa kuomba risiti pindi wanaponunua bidhaa hizo.
”Tuna kazi ya kufanya katika masuala ya kodi kwasababu tumeamua lazima tuwe taifa linalojitegemea si heshima kwa nchi kama Tanzania kutegemea misaada lazima kuweka nguvu katika ukusanyaji wa kodi ili tuboreshe huduma za jamii hivyo wauza bidhaa kutoa risiti na watu wanaonunua nao wadai risiti,”amesema Dkt.Nchemba
Aidha Dkt.Nchemba ameiagiza Ofisi ya TOST kuhakikisha inatatua migogoro mbalimbali ya kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato pamoja na kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Dkt. Nchemba amesema kuwa Serikali inatarajia kwamba Ofisi hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya kikodi na kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari, hivyo kuongeza mapato ya Serikali.