Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi ya vijana 268 ambao ni wanufaika wa Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) iliyofanyika katika eneo la Chinangali, Dodoma
Baadhi ya Vijana wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi ya vijana 268 ambao ni wanufaika wa Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) iliyofanyika katika eneo la Chinangali, Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akieleza namna wizara hiyo imejipanga kuendeleza vijana kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) wakati wa hafla ya mapokezi ya vijana 268 ambao ni wanufaika wa Programu hiyo iliyofanyika katika eneo la Chinangali, Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa neno la pongezi kwa vijana 268 ambao ni wanufaika wa awamu ya kwanza Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT), katika eneo la Chinangali, Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akikabidhi barua ya umiliki wa kiwanja pamoja na vitendea kazi kwa vijana 268 ambao ni wanufaika wa Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) iliyofanyika katika eneo la Chinangali, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli (kulia) akileza jambo wakati wa wakati wa hafla ya mapokezi ya vijana 268 ambao ni wanufaika wa Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) iliyofanyika katika eneo la Chinangali, Dodoma tarehe 22 Januari, 2024. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Na; Mwandishi Wetu – Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amehimiza ushirikiano baina ya ofisi hiyo na Wizara ya Kilimo ili kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya kilimo.
Prof. Ndalichako akizungumza kwenye hafla ya mapokezi ya vijana 268 wanufaika wa programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT), katika Shamba la pamoja la Chinangali II Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, amesema na serikali imeanzisha programu hiyo ili kupunguza tatizo la ajira, hivyo wakiwezeshwa kufanya kilimo biashara wataweza kujiajiri, kuajiri wenzao na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika pato la Taifa.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema vijana hao wa BBT wamekabidhiwa vifaa wezeshi vya kilimo pamoja na mashamba na wataanza na kilimo cha alizeti katika eneo hilo la Chinangali II.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameeleza kuwa programu hiyo ya Jenga Kesho Iliyo Bora itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa chakula nchini.