MKUU wa Majeshi ya Ulinzi(CDF) Jenerali Jacob Mkunda ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 5,000 za makazi kwa wananchi wanaohama kwa hiyari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro
Mradi huo unatekelezwa katika kijiji Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).
Akikagua mradi huo, Jenerali Mkunda amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo n namna Vijana wa JKT wanavyoutekeleza mradi huo kwa weledi mkubwa.
Aidha ametoa rai kwa watendaji wote katika mradi huo kuendelea kutekeleza mradi huo kwa uzalendo mkubwa ili uweze kukidhi na kufikia matarajio ya Serikali.
Pia Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda amewapongeza vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa na amewataka kuendeleza morali ya kufanya kazi kwani huo ndio moyo wa kizalendo kwa Taifa lao.