WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akizungumza wakati akizindua Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Adadi Mohamed Rajabu,akieleza malengo ya tume hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi ,ACP Emmanuel Mkilia,akitoa taarifa na mikakati ya tume hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,(hayupo pichani) wakati akizindua Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye, akizindua Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Adadi Mohamed Rajabu.Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah.
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akikabidhi Vyeti kwa wajumbe wa Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,ameitka Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi kusimamia majukumu ya Tume hiyo, kwa kuzingatia sheria katika kuhakikisha inalinda ,haki na utu wa watu wa taarifa ili kujenga imani kwa watu wote hasa wanaotoka nje ili waone Tanzania ni sehemu salama.
Waziri Nnauye ametoa rai hiyo leo Januari 19,2024 jijini Dodoma na mara baada ya kuzindua Bodi hiyo ambapo ameitaka Bodi hiyo kuanza kutoa elimu kwa umma kuhusu ulinzi wa Taarifa binafsi kupitia makongamano mbalimbali ili wawe na uelewa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah amesema kuwa alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano.
Awali,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi ,ACP Emmanuel Mkilia amesema wamekuwa na mpango mkakati wa siku mia moja ikiwemo kujenga uelewa katika ukusanyaji Taarifa kwa taasisi ambapo wameweza kufanikiwa.