Na Gideon Gregory, Dodoma.
Baadhi ya vyama vya upinzani Mkoa wa Dodoma ACT Wazalendo,ADC,NCCR Mageuzi,Cuf na Demokrasia makini vimetangaza kutokususia uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Akizungumza leoJanuari 18,2024 Jijini Dodoma kwaniaba ya vyama hivyo mbele ya waandishi wa habari mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma Yohana Mussa amesema suala la uchaguzi ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.
“Na hii ni kauli ya kiongozi wa chama Zitto, sisi hatutosusia uchaguzi na hatutoacha shamba la mihogo Nguruwe wakatafuna tutatafuta hata mishale mpaka Nguruwe huyo akaondoka, kimbembe kitakuja pale tumeshinda wakatangaza mtu nje ya vile tulivyoona tumeshinda,”amesema.
Katika hatua nyingine Vyama hivyo ambayo ni ACT Wazalendo,ADC,NCCR Mageuzi,Cuf na Demokrasia makini vimesema kuwa vinaunga mkono maoni ya Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Tume ya uchaguzi.
Miswada hiyo ni Muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa mwaka 2023 Muswada wa sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya malekebisho ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2023
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Stephen Chitema amewaka wabunge kuzingatia maoni yaliyotolewa kikao kazi juu ya mabadiliko ya katiba kwani jambo hilo ni la muda mrefu na limekuwa likitumia fedha nyingi.
Sambamba na hilo Chitema amesema maandamano ya tarehe 24 yameitishwa kwaajili ya wafuasi wa CHADEMA na wananchi, wakati ambao wananchi wapo mashambani wakiendelea na kilimo,
“Kwa wito huu wanataka wananchi watoke kwenye shughuli za kilimo waje mijini kuandamana hii sio sahihi, “amesema.
Amesema Mbowe anaitisha maandamano katika jiji la kibiashara dar uku akitambua juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua frusa za uwekezaji na biashara katika jiji ilo.
“Sisi Wenyeviti wa Vyama Vya Upinzani Tuliopo Makao Makuu ya Nchini Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Uamuzi Wake wa Kupeleka Bungeni Marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambapo sasa, kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria chini ya mwenyekiti wake Joseph Mhagama imetoa fursa kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao wakiwao CHADEMA nafasi kwa wadau kutoa maoni yao kila mmoja kwa nafasi yake,
Amesema kamati ya bunge ilitoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau kiasi cha kutosha ilifikia baadhi ya wadau walipewa nafasi Zaidi ya mara moja kutoa maoni yao wakiwamo hawa wanaitisha maandamano
“Chama cha Chadema na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe imekuwa ni tabia yao kuacha michakato halali na kukimbilia kwa wananchi kujilizaliza, Sisi wenyeviti himala tunasema atuungi mkono maandamano hayo na tunalaani kwa nguvu kubwa ukiukaji huu wa maridhiano ya demokrasia yalianzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ” amesema.